Tanzania Bureau of Standard (TBS)

Tanzania Bureau of Standard (TBS)

Mwenezi ACT

Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
36
Reaction score
7
Hivi karibuni pamekuwepo na malalamiko mengi sana ya kutapeliwa kwa baadhi ya watanzania wanaoshirikiana na makampuni ya nje kibiashara, ni changmoto ambayo imekuwa ikiwakumba raia wengi wa Tanzania juu ya makampuni ya kitapeli ya kigeni wanayo fanya nayo biashara.

Ni ukweli usuo na kificho kuwa pamekuwepo na makampuni mengi ambayo yameanzishwa kwa nia zisizo njema ili kuwaibia watanzania.Imekuwa ni desturi kwa watanzania kusikia makampuni hewa yakiingia mikataba mikubwa na taasisi kubwa za Serikali na kulitia taifa katika umasikini kutokana na ubadhilifu wa matrilioni ya fedha.
Kiini cha matatizo yote haya ni kuwa na utaratibu mbovu wa ufuatiliaji wa kina kwa makampuni ambayo taasisi yanaingia nayo mikataba ama kuwa na watendaji wasio waaminifu ambao wanatumia mwanya huu kama chujio la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Mwaka jana Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilitangaza Tenda ya ukaguzi wa ubora wa uingizwaji wa magari kutoka nje ya nchi, ambapo katika tenda hiyo yaliwasilishwa malalamiko dhidi ya kampuni ambayo kwa asilimia kubwa ilikuwa ikitia mashaka juu ya utendaji wake kazi sambamba na taarifa za kampuni hiyo ambazo zinapatika katika vyanzo mbalilmbali.

Hivi karibuni tumeshuhuduia rasmi madudu ya aibu ya mwaka katika kutoa zabuni hiyo kwa kampuni isiyo na sifa hata kidogo, kampuni hiyo iitwayo Serengeti Global Services Limited. Kwani katika tenda hiyo kampuni hiyo ya Serengeti ilibainika kwa yauatayo:-
I. Kutokuwa na rekodi yeyote ya utendaji kazi wake katika kazi, kwani katika object clauses za kampuni hiyo
hawaja ainisha kama wanashughulika na swala hilo.
II.Walishatajwa kuwa wana ushirika wa karibu na kampuni ya Utility ambayo awali ilipatiwa tenda ingawa haikuwa
na vigezo vya tenda hiyo.
III.Kampuni ya Serengeti Global Services Limited kutokuwa na taarifa za fedha ambazo zimekaguliwa kwa mfululizo
wa miaka mitatu.
IV.Kuwa na taarifa za fedha ambazo hazionyeshi on going concern kwa kutoweka wazi faida ambayo kampuni inapata.
V. Kuwasilisha taarifa zaumiliki wa fedha zenye thamani ya dola za kimarekani 20,000/= katika benki ya Azania
nchini Tanzania, jambo ambalo halijaonyeshwa katika taarifa zao zaredha za kila mwaka kama wana miliki fedha
nje ya nchi.
VI.Kutokuwa na vigezo vya kupatiwa zabuni kwa mujibu washeria za PPRA
VII.Miongoni mwa wamiliki wake walisha kutwa na makosa ya drug traffic na kutumikia kifungo gerezani.
Ni jambo la kushangaza kuwa pamoja na kasoro hizi Shirika ka Viwango la Tanzania ( TBS) limeweza kutoa zabuni hiyo kwa kampuni ya Serengeti Global Services Limited, jambo ambalo ni limekuwalikiumiza kichwa changu kwa mda mrefu sana kwani nakosa imani hata na bidhaa zinazo kaguliwa na TBS.

Katika kufuatilia historia vizuri ya wamiliki halali wa kampuni ya Serengeti Global Services Limited ni kuwa Ndugu, Christopher Lukosi ambaye ni mkurugenzi wa kampuni hiyo alikuwa nia mwenyekiti wa CHADEMA nchini Uingereza, nadhani hii ndiyo ilikuwa sababu rasmi ya Nguli huyu wa CHADEMA kuota mbawa na kujikuta yuko Kizota.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki ACT.
 
Back
Top Bottom