Tanzania bila umaskini haiwezekani

tegulirwa

New Member
Joined
May 13, 2009
Posts
1
Reaction score
0
Habari ya leo watanzania. Nina andika hoja hii kwa kuangalia mijadala mbalimbali na namna watu tunajenga hoja kuhusu kutatua jambo fulani la kijamii. Mtizamo wangu, ni kuwa tumekuwa watu wa kutupia mzigo kwa mtu, taasisi na hata serikali kwa mwingine.

Mfano nimesikiliza mjadala jana katika ITV kujadili namna ya kuwasaidia watoto wetu wanafunzi waweze kufika shule bila usumbufu na kulelewa katika maadili ya kitanzania enzi hizo. kwasasa tunaimba hiki kizazi cha dotcom hakisikii hata kidogo. nashawishika kusema hata washiriki waliokuwa katika mjadala mzima wa wadau, hakuna ambaye aliyekuwa akijaribu kutoa suruhisho bali lawama kwa mtu mwingine.

Naomba niwarejeshe huko, mwenye maoni achambue na kuja na suruhisho.

Mimi mchango wangu ni kama ifuatavyo, biashara ya usafiri mijini nisawa na biashara nyingine kama tunahitaji biashara stahiki ni lazima tukubali kulipia gharama za uendeshaji na nauli kama inavyoelekezwa. ninapinga serikali kuja na nauli ya mwanafunzi kwa sababu zifuatazo. sija wahi kusikia mwanafunzi akipanda bodaboda anauliza nauli ya mwanafunzi, akipanda taxi anauliza nauli ya mwanafunzi, akipanda bajaji anauliza nauli ya mwanafunzi, akipanda ndege au basi la mkoani anauliza nauli ya mwanafunzi.

hawa fanyabiashara ya daladala wanawekeza mitaji yao, wanakopa benki na kupewa riba kama wengine; ni kwanini hili kundi liwe suruhisho la kubeba matatizo yetu na wao watabebewa na nani? tukienda mbali zaidi sijasikia mwanafunzi akienda dukani anaomba bei ya mwanafunzi, sokoni, kununua ice cream, kununua chips kibandani kote huko hakuna bei ya mwanafunzi, iweje kwenye daladala. Kama wazazi tunawapenda watoto wetu na kuwathamini tuwalipie nauli kamili usafiri utakuwa ni mzuri watafika kwa wakati na makonda watawakimbilia kama mpira wa kona. magari ya staha yataongezeka. wazazi tubebe mzigo wetu.

Hapa nina kwenda mbali zaidi, hata kwa watumishi wanaoombewa ruhusa wasafiri bure kwenye daladala, hii ni ajabu kweli kweli. Mzigo huo anatwishwa mfanya biashara ya daladala. Kama serikali inawaonea huruma ongeza mishahara upatikane unaokidhi mahitaji. na siyo kuomba wasafiri bwelele. wote tunalipa kodi, TRA hana simile kuwa huyu anasafisha bure akina so and so, kama tunawaonea huruma saaana, wapewe haki yao ya mshahara unaotoshereza.

Hitimisho langu ni kuwa tukiendelea na mawazo haya tunaleteana umaskini na umaskini hautaisha hapa Tanzania.
 
Habari ya leo watanzania. Nina andika hoja hii kwa kuangalia mijadala mbalimbali na namna watu tunajenga hoja kuhusu kutatua jambo fulani la kijamii. Mtizamo wangu, ni kuwa tumekuwa watu wa kutupia mzigo kwa mtu, taasisi na hata serikali kwa mwingine
Hata wewe mwishoni hapo umetumia mzigo na lawama, watu, viongozi, au taasisi Fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…