Poise
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 7,633
- 7,901
Hivi mmeelewa maudhui ya mwandishi na kwa nini ameruka ruka kuelezea utawala wa Mkapa na Kikwete? Halafu huyo akaanza kushikilia bango sheria ya madini.
Chamoto ,.
Mkuu
Rais Dr Magufuli, ndiye tunamhitaji.
Rais, Putin wa Russia amewakomalia wazungu koko hadi sasa hivi uchumi wa Russia unapaaa ile mbaya na ile nguvu ya Russia wakati wa USSR inaanza kurudi kwa kasi ya umeme.
Mfano, ulidhania kuwa USA atafukuza baadhi ya wanadiplomasia wa Russia kutoka USA kisha Russia ijibu mapigo kwa kuwaondoa wanadiplomasia wote USA nchini mwake (Russia)!!
Kwa hiyo, wazungu koko hawataki mtu anayewawekea USO wa mbuzi pale wanapoiba raslimali za nchi husika.
Wanapenda wakutane kila siku na rais dhaifu na viongozi waandamizi wa serikali walio goigoi ili washerekeee huko ulaya wakati sisi huku Africa and Tanzania tubakie kulialia na kuombaomba.
Kwa ujumla, watanzania tunahitaji kuondoa tofauti zetu na itikadi zetu za kivyama kisha kusimama pamoja na serikali yetu kwa ajili ya manufaa ya Tanzania na watanzania.
Vinginevyo tutakuwa shamba la bibi kwa kila kikaragosi kuja kuvuna na kuondoka kwenda kula mema huko kwao.
Tanzania mpya inawezekana ...