Pius Kafefa
Member
- Aug 9, 2011
- 88
- 20
Wadau nimeamua kuandika haya kutokana na ukweli wa hali inayoelezea kipindi tunachopitia Watanzania. Kipindi hiki kilianza wakati wa awamu ya nne ya utawala chini ya Rais J. M. Kikwete, na kitaendelea hadi mwaka 2020. Tukiitazama Tanzania kabla ya mwaka 2005, ni wazi tutaona jinsi ilivyokuwa tofauti kisiasa, kiuchumi, na kijamii na Tanzania iliyoko kwenye kipindi cha mpito.
Sababu za Tanzania kuingia kwenye kipindi cha mpito:
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Sababu za Tanzania kuingia kwenye kipindi cha mpito:
- Utawala wa kisiasa ulioshika dola kuanzia mwaka 2005 ulibadili mfumo wa kiutawala ili kuweka watu waliokuwa wakiuunga mkono uongozi huo. Kipindi hiki ndicho kilichoshuhudia utawala ukilaumiwa kwa kuweka watu kwenye system kishkaji. Waliokuwa kinyume na status quo walipoteza nafasi zao. Kipindi hiki kimeshuhudia mnyukano mkali na wa wazi ndani ya chama tawala kiasi cha kukaribia kumeguka kufuatia kuibuka kundi lililokuwa likipinga ufisadi, huku wanachama wengi wa chama tawala wakiona hakukuwa na tatizo. Hadi leo, mambo ndani ya chama tawala hayajatulia kutokana na harakati za kisiasa kuelekea 2015.
- Vyama vya upinzani vilivyokuwa vimebadili uongozi viliweka watu wapya waliokuja na mbinu mpya za kufanya siasa. Siasa ya upatanisho na dola au chama tawala ilikoma na kuingia siasa ya kushambuliana kupitia kashfa mbalimbali kama za wizi wa EPA, mikataba ya kifisadi, wizi wa fedha za halmasauri, na wizi wa kura wakati wa uchaguzi. Uchaguzi mkuu wa 2010 umeshudia Chadema ikiongeza wabunge kutoka 5 (2005) hadi 44 (2010) huku ikionywa na chama tawala na wachambuzi wengine iachane na siasa za kiharakati.
- Kutikiswa kwa umoja wa kitaifa. Kwa mara nyingine ufa kwenye muungano wa Tanganyika na Zanzibar umekolezwa kutokana na uwepo wa maridhiano ya CCM na CUF. Maridhiano hayo yamewafanya Wazanzibari kuwa na sauti moja linapokuja suala la maslahi ya Zanzibar, hali iyopelekea kutokea kwa hoja ya kurudisha serikali ya Tanganyika wakati wa mchakato wa kuandika katiba mpya. Umoja wa kitaifa umetikiswa pia na vuguvugu za kidini ambapo wakristo na waislamu wamepungukiwa na uvumilivu. Tayari kuna mauaji yameshatokea kutokana na hili, na hakuna juhudi za kuridhisha zinazofanywa kushughulikia tatizo la kidini.
- Kadhalika, siasa za kizazi kipya zimebadili mfumo wa uendeshaji wa harakati za kisiasa ambapo vyama vya siasa vinalazimika kuwa na mtandao wa vyombo vya habari kwa ajili ya kufanya propaganda. Kwa sasa imekuwa vigumu kuamini moja kwa moja taarifa zinazopashwa kuhusu chama fulani kwani vyombo vingi vya habari (pamoja na waandishi wake) vinaegemea kwenye maslahi ya kisiasa. Hili linathibitika kirahisi kwa kupitia 'headlines' kwenye magazeti ya kila siku au kila wiki.
- Vyama vya upinzani viendelee na siasa za kiharakati bila kulala (vikilala kitafuata kipindi kigumu cha maangamizi ya wafuasi wake).
- Chama tawala kianze kujipatanisha na tabaka la maskini ambao ndio wengi katika nchi hii. Kisipofanya hivi kitaendelea kukataliwa na kutegemea mbinu muflisi za kupakana matope.
- Watu wote maarufu wa nchi hii waheshimiwe bila kujali itikadi au mitazamo yao katika baadhi ya mambo yanayotokea katika nchi hii.
- Maoni yenye mtazamo wa kisiasa yaheshimiwe pale yanapotolewa na Watanzania ambao hawaishi kwa kufanya siasa. Watnzania hawa wanaweza kuwa ni wanafunzi, wafanyakazi, wanataaluma, wamachinga, madereva wa bodaboda, n.k.
- Baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 chama kitakachotawala kiendelee na ujenzi wa taifa jipya lenye amani na watu wenye upendo, utulivu, na mshikamano bila kujali itikadi zao za kisiasa, kidini na tabaka atokalo mtu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.