TANU Iliasisiwa na Watu Waliokuwa na Uzalendo wa Kweli

TANU Iliasisiwa na Watu Waliokuwa na Uzalendo wa Kweli

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
CHAMA CHA TANU KILIUNDWA NA WATU WENYE UZALENDO WA KWELI NA NDIYO SABABU YA KUWA NA NGUVU KUBWA
Msikilize Mwalimu Nyerere anavyoieleza nguvu kubwa ya chama cha TANU:


View: https://youtube.com/shorts/SdMP_ZD6zUQ?si=F-6u0yrWVpQVumIn

Video ina changamoto lakini Mwalimu anasema TANU ilikuwa haina mpinzani na ikishinda kila uchaguzi.

Mwalimu kaeleza kwenye hiyo video nguvu ya TANU katika uchaguzi na kautaja uchaguzi wa rais wa mwaka wa 1962.

Uchaguzi huu TANU ilipambana na Zuberi Mtemvu wa Congress.
Congress ilishindwa vibaya sana.

Picha hiyo hapo chini Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mabwana wako na Nyerere nje ya Ukumbi wa Arnautoglo wamemsindikiza Mwalimu siku ya kupiga kura.

1754405229752.jpeg

Kulia: Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi.

Picha hii imechapwa na Daily News lakini katika maelezo ya picha jina lililoandikwa ni la Nyerere peke yake.

Mshume Kiyate na Max Mbwana wamepewa Mtaa kila mmoja.

Wahusika huu unapata kuwa mwaka wa 30 wamekataa kubadili mtaa na kuweka vibao vya majina ya wazalendo hawa.

1754405331764.jpeg

Kulia: Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere, John Rupia miaka ya mwanzo ya TANU nyuma ni Bantu Group wahamasishaji na walinzi wa viongozi na waliosimama wa pili ni Ali Msham.

Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu.
Wenye mamlaka wamekataa kumpa mtaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom