Fanyeni kazi mpate maisha mazuri. Huu upuuzi wa kulilia jina utawasaidia nini? Wakati mnahangaika kuitafuta Tanganyika, wenzetu wa akili finyu wameishia kwenye bodaboda. Huku nyuma ardhi inapokwa na wageni na watu weupe. Ninyi badala ya kuhanagikia uchumi, mnalilia "jina". Haya, na kesho iwe Tanganyika, watoto wetu ada zitapunguzwa shuleni? Watapata mlo sahihi? Watatibiwa kama anavyostahili binadamu kutibiwa? Mtapata maji kwenye mabomba? Acheni ujuha. Iwe Tanzania, iwe Tanganyika, bila kujibidisha kwa haki, na kupambana na hawa majizi wa mali za umma, ni kazi bure.
Nawasilisha
Manyerere