TANESCO yaomba kuongeza bei ya umeme

TANESCO yaomba kuongeza bei ya umeme

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
6,999
Reaction score
1,187
Baada ya kuwasilisha maombi yao rasi Ewura, mamlaka hiyo nayo imetoa tangazo lifuatalo:​



TANGAZO KWA UMMA
WITO WA KUKUSANYA MAONI YA WADAU KUHUSU OMBI LA TANESCO LA KUPANDISHA BEI YA HUDUMA YA UMEME

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea ombi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinishiwa ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari Mosi, 2011. TANESCO wanaomba bei za huduma ya umeme ziongezeke kwa asilimia 34.6 kwa mwaka 2011; asilimia 13.8 mwaka 2012; na asilimia 13.9 mwaka 2013.

Kulingana na Kifungu Na.19 (2) (b) cha Sheria, Sura 414 ya Sheria za Tanzania, EWURA imeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu uhalali wa ombi lililowasilishwa na TANESCO. Ili kufikia malengo hayo, EWURA inawakaribisha wananchi wote kuhudhuria na/ama kuwasilisha maoni yenu katika mikutano itakayofanyika katika mikoa na tarehe mtakayojulishwa baadaye.

Kulingana na kifungu Na. 10(1) cha Mwongozo wa Uwasilishaji Maombi ya Bei wa Mwaka 2009 (Tariff Application Guidelines of 2009), wanachi wote wanaotaka kuweka pingamizi kuhusiana na ombi tajwa wanatakiwa kujiandikisha EWURA kabla ya saa 11:00 jioni siku ya Jumatano tarehe 14 Julai 2010. Wale watakaojiandikisha watapewa fursa ya kuwasilisha maoni yao katika mikutano husika. Wadau wengine ambao hawatajiandikisha pia watapewa fursa ya kutoa maoni yao papo kwa papo katika mikutano hiyo. Ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya mikutani husika, wadau watapewa fursa ya kuwasiliasha maoni yao kwa maandishi kuhusiana na maombi husika wakati wowote kabla ya saa 11:00 jioni.

Pamoja na nakala ya ombi husika kupatikana bure katika tovuti ya EWURA (www.ewura.go.tz), isipokuwa nyaraka za siri zilizowasilishwa EWURA na mwombaji kulingana na kifungu cha 25 cha Sheria, Sura 414; nyaraka nyingine zote zilizowasilishwa zinapatikana katika ofisi yetu katika annuani hapo juu kuanzia saa tatu (3) asubuhi mpaka saa 11:00 jioni. Hata hivyo wadau watakaohitaji nakala za ombi hilo wanaweza kupata kwa kulipa kiasi cha TZS 25,000 ikiwa ni gharama za kudurusu nakala hizo. Pia, unaweza kusoma maombi hayo bure wakati wa kazi katikq ofisi za EWURA.

Kwa maelezo zaidi tuandikie kwa anuani hapa juu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU,
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea ombi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinishiwa ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari Mosi, 2011. TANESCO wanaomba bei za huduma ya umeme ziongezeke kwa asilimia 34.6 kwa mwaka 2011; asilimia 13.8 mwaka 2012; na asilimia 13.9 mwaka 2013

Waelekeze nguvu kwenye kukusanya madeni kwanza na kudhibithi wizi. Hizi shortcuts za kupandisha bei watatumaliza!
 
Yaani thinking capacity ya viongozi wa TANESCO imeishia hapo?? Ni ajabu kweli!!! Kwa nini wanasua sua kuipa ruhusa kampuni ya atumas ili izalishe na kusambaza umeme huko kusini?? Kuna nini?? Yote haya ya kupandisha hovyo bei ya umeme ni uvivu wa kufikiri na kutafuta vyanzo mbadala vya mapato.

Katika afrika tanzania ndo nchi yenye umeme wa ghali sana lakini jamaa wsivyo fikiria wanaona njia pekee ya kufidia gharama za mikataba ya kijinga ya IPTL, SONGAS, Kiwira, ni kupandisha bei?? Hovyo kabisa.
 
Ndio maana watu wanajishughulisha na numeme wa wizi, lazima watafute dawa ya matatizo, kupandisha bei ni short term solution,
 
Yaani thinking capacity ya viongozi wa TANESCO imeishia hapo?? Ni ajabu kweli!!! Kwa nini wanasua sua kuipa ruhusa kampuni ya atumas ili izalishe na kusambaza umeme huko kusini?? Kuna nini?? Yote haya ya kupandisha hovyo bei ya umeme ni uvivu wa kufikiri na kutafuta vyanzo mbadala vya mapato.

Katika afrika tanzania ndo nchi yenye umeme wa ghali sana lakini jamaa wsivyo fikiria wanaona njia pekee ya kufidia gharama za mikataba ya kijinga ya IPTL, SONGAS, Kiwira, ni kupandisha bei?? Hovyo kabisa.

Nimechukia sana nashindwa hata kuandika..... will be back
 
Reliable power supply is very crucial for the well being and development of the country as a whole. Having such a reliable power would lead to development in all other sectors through local/foreign investments. With the current situation in Tanzania it is very inappropriate to request for a price increase for the very poor quality and unreliable electricity. EWURA as a regulatory authority is responsible for quality and standard of energy/water supply from utility companies, but to my surprise they are only concerned with prices. Is it because they get a percentage from TANESCO for every sale of unit (kWh)? Together EWURA and the Utilities have become rip off artists….they rob Tanzanians on broad day light? WTF?????????

Things that are done in Tanzania are just unbelievable. The country has a problem with every service it is supposed to render to the citizens. Raising power tariffs is just a very bad move. TANESCO has lots of uncollected debt and since they have failed in debt collection they are trying to shift the load to the poor exploited citizens who experience load shedding for more than ¾ of a year!!? Theft is their norm of the day and yet they say running costs are high!! No new investments and you always think of doing projects that are unrealistic like building a gas turbine generator in Mwanza – how will u get the gas to that stupid white elephant project in Mwanza? Damn you people….

At the moment only 10% of the country is electrified with the poor quality and unreliable power. The remaining 90% have no dream of using electricity at least in their period of living in this world!! I pity my relatives in the rural since they are the victims of such bad leadership!
 
WAKATI wananchi wanalalamika kuwa gharama za umeme ziko juu na huduma zake kutokuwa za uhakika, Tanesco inakusudia kupandisha bei kwa asilimia 34.6 mwishoni mwaka huu.

kwa sasa bei za umeme ni kama ifuatavyo.

Tariff D1 ( Domestic Tariff) 50 units Tsh 49/unit na kila inayozidi kama unatumia Tariff D1 ni sh 156/unit

Tarrif T1 (Domestic/Commercial) matumizi ni >=283kWh/month na kila unit ni Tsh 129 Plus Service charge ya Tsh 2303/month

Hizi ndo tariff zanazotuhusu sisi walala hoi....kuna tariff T2 na T3 kwa ajili ya viwanda mabao hao huchajiwa kwa KVA. hawatuhusu sana.

New cost kama EWURA watapitisha maombi ya Tanesco itakua kama ifuatavyo

Tariff D1 Tshs65.95/unit for first 50 units na kila unit itakayozidi itakua 210/unit
Tariff T1 Tshs 173.65/Unit na service Charge

Bei zote hazina VAT wala 1% ya EWURA

JE TUTAFIKA???

Nawasilisha
 
Sikuhitaji kusoma tundiko zima kwa sababu hapo juu tu nikajua we mwongou, ukweli naujua. Kwa nini niendelee kusoma taarifa za mwongo?

Don't judge a Book with its Cover; Tafadhali soma tundiko zima upate mada nzima; Naamini muwasilishaji hajapotosha umma, nimefuatilia kwenye vyombo vya habari jamaa wameomba kupandisha kwa awamu.

kazi kwelikweli:

Maisha Bora ZAIDI=kasi mpya zaidi,nguvu mpya zaidi,hari mpya Zaidi
 
................kerosene ni approximately 1400 TShs. kwa lita. Misitu kwa heri maana ni mwendo wa kuni na mkaa!!!
 
Don't judge a Book with its Cover; Tafadhali soma tundiko zima upate mada nzima; Naamini muwasilishaji hajapotosha umma, nimefuatilia kwenye vyombo vya habari jamaa wameomba kupandisha kwa awamu.

kazi kwelikweli:

Maisha Bora ZAIDI=kasi zaidi,nguvu zaidi,hali Zaidi
Sawa wemeomba kupandisha je watapandisha bei au hawapandishi! maana siyoni sababu ya msingi kumshambulia jamaa,kwa sababu nijuavyo hawa tanesco wana wakumzuia asipandishe, mi sijui tuendako maana huduma mbovu na unataka kuongeza bei kwa lipi haswa?
 
Habari wakuu,

Haya, kwa wananchi wa Tanzania, wenye maisha bora kuliko wote, wanaopata mlo 5 kwa siku, nyumbani mabomba ya maji yakitoa juice na maziwa, maisha ya raha kabisa, wankuja kuletewa hii mpya, ambapo tanesco imeona mnaishi kwa raha sana, kwa hiyo angalau iwapandishie ka bei ka umeme ili mjue maana ya maisha magumu. Tanesco imeamua kupandisha bei this year.

Jamani i am asking you fellow tanzanian,when people are soo poor,the facility is soo poor,sometimes no electricity at all,is this feasible? Yaani hawa jamaa kila mwaka wanapandisha bei, lakini shirika lina zidi ku nose dive, why?

We have the most expensive electricity in this region of south and East Africa, may be the whole Africa, and we have the worst economy in the same, so why keep torturing us? Jamani,when will we enjoy life in our own country? Why why why just we Tanzanians suffering?

We have gas, we have rivers, we have lakes, we have coal, what else do we need? Opposite should be the case,where tanzania should have the cheapest electricity in africa,but as they say,miafrika ndivyo tulivyo.
 
Yaani thinking capacity ya viongozi wa TANESCO imeishia hapo?? Ni ajabu kweli!!! Kwa nini wanasua sua kuipa ruhusa kampuni ya atumas ili izalishe na kusambaza umeme huko kusini?? Kuna nini?? Yote haya ya kupandisha hovyo bei ya umeme ni uvivu wa kufikiri na kutafuta vyanzo mbadala vya mapato.

Katika afrika tanzania ndo nchi yenye umeme wa ghali sana lakini jamaa wsivyo fikiria wanaona njia pekee ya kufidia gharama za mikataba ya kijinga ya IPTL, SONGAS, Kiwira, ni kupandisha bei?? Hovyo kabisa.
Hawa tanesco ni wapuuzi sana, badala ya kukusanya outstanding debts wao wanawaongezea gharama wateja waaminifu ndio maana sasa hivi watu wengi wanatumia umeme kinyemela bila kulipia. Inabidi waweke mkakati wa kuhakikisha kuwa kila unit moja inayozalishwa inalipiwa tofauti na sasa ambapo unit zinazolipiwa ni chini ya asilimia 50, sasa ndio nakisi inalazimishwa walipe loyal customers. very stu.pid
 
unajua hakuna kitu kizuri kama kua na mipango sahihi ? mi nashindwa kuelewa ni nini kinacho wafanya wapandishe bei? wakati waliondoa IPTL na kuweka ges ili kupunguza garama. mimi nilikua nategemea kusikia wana punguza pei kwani wanauziwa gesi kwa bei ya chini sana na najua asilimia kubwa ya umeme wetu una tokana na maji je hayo maji yamepanda bei?

minawashauri hizo wanazo sema garama zaundeshaji wanaweza kupata kutokana na watumiaji umeme wanao tumia bila kulipa waache kutuonea sisi wanyonge.

uhakika upo kua ofisinyingi za serikili hazilipi umeme na yumba nyingi za wakubwa hawalipi umeme.
je hawaoni kukuwa na mkakati wakukusanya hayo madeni ita saidia ?

Busara zinahitajika ilikuweka mipango ,
 
Back
Top Bottom