KERO TANESCO wekezeni katika Teknolojia, inachukua muda gani kurudisha Units baada ya kubadilisha Mita?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimevurugwa sana.
IKO HIVI.

Hapa napoishi tulikuwa tukitumia mita ya zamani, sasa TANESCO Tanzania walikuja na kuibadilisha na kuweka mpya, ile ya zamani ilikuwa na Units zaidi ya 80, na Units nyingine zilikuwa zimenunuliwa lakini hazijawekwa kwenye Mita.

Mafundi wa TANESCO baada ya kufanya yao, wakatuambia umeme uliokuwepo na huu ambao haujaingizwa tufuatilie kwenye ofisi za TANESCO za karibu. Kweli tulifuatilia ikiwa ni pamoja na kuandika maelezo kadili walivyotaka.

Sasa ni mwezi hakuna Units zilizorudishwa, ukifuatilia unaambiwa sijui Meneja hayupo, mara Mhasibu kafanya vile, imekuwa usumbufu mkubwa maana unaacha kazi zako, unafuatilia haki yako halafu unajibiwa tu kirahisi. Shirika bado linafanya kazi kwa mazoea tu kusumbua wateja. Shenzi sana.

Kama maelezo tumeweka, ushahidi wote tumeweka, nini kinawashinda kuturudishia huo umeme ili tuendelee kuwaza mambo mengine? Au kwasababu wao wana upendeleo wa units wanaona maisha rahisi sana.

Nimechukia sana.
 
POLE SANA. HUU NI UZI WA PILI KUHUSU HAYA MALALAMIKO. KUNA MTU PIA ALIWAHI KUTOA MALALAMKO KAMA YAKO KWENYE JUKAA HILO.
 
Kama kuna taasisi ipo nyuma ya wakati ni hao tanesco. Hivi inakuaje ununue umeme wa mita flani halafu uanze kutafuta kikaragosi chao kile uanze kubonyeza namba?
Vimashine vyenyewe batan zake mbovu.
TANESCO BADO MPO NYUMA YA WAKATI
 
Hiiii! kumbe wao wanapewa units za upendeleo?
Ila hata hivyo wana uzi wao wa tag watakusaidia mi niliweka shida yangu kwao wakanitafuta ikawa solved maana shida ilianzia juu ikaja chini nahisi shida yangu ali ipata mkuu wao jambo likaisha fasta.
 
Back
Top Bottom