TANESCO: Tutatoa taarifa rasmi tukimaliza kutumbuana

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuufahamisha Umma kuwa liko katika hatua mbali mbali za mabadiliko ya Uongozi wa ndani ya Shirika kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi.

Kwa msingi huo, mabadiliko yanayoendelea ndani ya Shirika yatawekwa wazi kwa wakati muafaka kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Shirika kwa kupitia vyombo vya habari.

Hivyo tunaomba vyombo vya habari vitoe fursa kwa Mamlaka husika kuendelea kukamilisha zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla na taarifa rasmi itatolewa baada ya zoezi kukamilika.

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO - MAKAO MAKUU
05 Januari 2017
 
Hii nchi imekuwa sio ya utendaji bali imekuwa ya kutafutana na kuviziana ili uonekane unafanya kazi
Hivi watu wengine mna akili timamu kweli ? Kila kitu mnaona hakifai mnataka nn hasa ? Maboresho yanayofanywa ili kuboresha ufanisi mnaona ni upumbufu au ndiyo mnalipwa kukosoa ? Tangulizeni uzalendo na siyo hizo posho mnazopewa kukosoa kila jambo
 
Sio kwa Tanzania hii
 
Sasa ukifanya kazi kwenye mashirika ya umma unabidi mkobani utembee na hati ya mahakama kama zuio la kutotumbuliwa kwa hali yoyote ile. Wakitangaza tu wamekutumbua unaweka hati goto mezani, wanaufyuata,mwendo unakuwa ni mahakamani salaries unaendelea kuvuta salary yako.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuufahamisha Umma kuwa liko katika hatua mbali mbali za mabadiliko ya Uongozi wa ndani ya Shirika kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi.

Kwa msingi huo, mabadiliko yanayoendelea ndani ya Shirika yatawekwa wazi kwa wakati muafaka kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Shirika kwa kupitia vyombo vya habari.

Hivyo tunaomba vyombo vya habari vitoe fursa kwa Mamlaka husika kuendelea kukamilisha zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla na taarifa rasmi itatolewa baada ya zoezi kukamilika.

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO - MAKAO MAKUU
05 Januari 2017
Tupe uthibitisho kama hicho ulichoandika kina ukweli ,tutaaminije kiongozi
 
Hivi watu wengine mna akili timamu kweli ? Kila kitu mnaona hakifai mnataka nn hasa ? Maboresho yanayofanywa ili kuboresha ufanisi mnaona ni upumbufu au ndiyo mnalipwa kukosoa ? Tangulizeni uzalendo na siyo hizo posho mnazopewa kukosoa kila jambo
Binadamu tunatofautiana kimtizamo, anavyowaza mwenzako ni tofauti na uwazavyo ww. Kwahiyo si vyema kmkejeli mwingine sijui ana akili ama vp. Jukwaa hili linatakiwa kujengwa kwa hoja sio kejeli wala matusi
 
Hakuna hoja yoyote ya maana kwenye hii thread zaidi ya mihemko. Mojawapo ya sehemu za kufanyia utafiti wa elimu ya tz kama ni bora au bure kabisa ni humu ndani ya jukwaa. Watu hawana hoja wala hawachangii kwa hoja bali ushahabiki au kulaumu tu bila kuonyesha kwa undani logic ya kushahabikia au kulaumu kwake
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuufahamisha Umma kuwa liko katika hatua mbali mbali za mabadiliko ya Uongozi wa ndani ya Shirika kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi.

Kwa msingi huo, mabadiliko yanayoendelea ndani ya Shirika yatawekwa wazi kwa wakati muafaka kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Shirika kwa kupitia vyombo vya habari.

Hivyo tunaomba vyombo vya habari vitoe fursa kwa Mamlaka husika kuendelea kukamilisha zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla na taarifa rasmi itatolewa baada ya zoezi kukamilika.

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO - MAKAO MAKUU
05 Januari 2017
Sio rahisi kwa sababu ni hatari sana.. Ili umeme usafiri kwenye hewa utahitaji nishati(energy) kubwa ambayo itabadilisha air into plasma ambayo ndio itaweza kusafirisha umeme.. Ambapo huwa ni approximately 30,000 volts per 1 cm.. Sijui unaelewa.. Huo ukipigwa nao unakua majivu.. Hahah
 
Back
Top Bottom