TANESCO mnatuibia!

Ila kusema kweli hii nchi imeoza sana.Halafu bado kuna mambumbumbu humu JF wanatetea upuuzi wa serikali ya Chama cha Mamburula kisa tu wanapewa buku saba.
 
Umeme unakwenda sana mm natumia kwa siku unit 8 na nyumba yakawaida tu taa na tv hata feni situmii nipo karibu na beach sasa sijui nini tatizo

Wezi sana hawa! Halafu sasahivi wameanza na mfumo wa kufunga mita juu ya nguzo ya umeme hata kwa watumiaji wa umeme wa mkondo mmoja (single phase)
 

Hivi capacity charges si ilikuwa ni ya miaka 20 au nakosea? Maana yangu ni kwamba sio ya kudumu hata ikinunuliwa na mtu mwingine, sana sana huyo mwingine anapata investment relief? Au ndio kizungumkuti chenyewe?
 

Kama unatumia UMEME chini ya Unit 70 kwa mwezi na umetumia zaidi ya miezi 3 andika barua kwa Tanesco na upeleke kwenye office zao za mkoa uliopo watakubadilishia Tariff.
 

Yes, wangeweka option ya mteja kuchagua tarrif anayoitaka toka mwanzo. Na mita zao wangetofautisha yaan ziwepo za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa. Za mtumiaji mdogo zingesetiwa kuwa ziwe zna limitation ya kutojaza unit zaid ya 75.
 
Hivi capacity charges si ilikuwa ni ya miaka 20 au nakosea? Maana yangu ni kwamba sio ya kudumu hata ikinunuliwa na mtu mwingine, sana sana huyo mwingine anapata investment relief? Au ndio kizungumkuti chenyewe?

Nafikiri ipo hivo. Na hilo halina ubishi; Watanzania wote ambao ni wateja wa TANESCO km mimi na wewe tunalipia hiyo capacity charge kila mwezi kupitia SERVICE CHARGE tunayotozwa. Wewe fikiria kila mwezi unalipia Tsh 6734; ushajiuliza kwanin unalipia pesa hizo wakati unalipia energy charge ambayo ni Tsh 375 kwa unit? Hawa jamaa ni MAFISADI wa kupindukia!
 
Let's kokotoa matumizi kwa siku:
Kifaa Power(kw) Muda(hrs) unit
Fridge 0.3 10* 3
Taa 5 0.2 5 1
TV. 0.15. 5 0.75
Pasi. 2. 0.2. 0.4
Jumla ya units kwa siku. 5.1

*Fridge kwa wastani lina nguruma chini ya dakika 30 kwa saa 1(on off operation) Hivo kwa masaa 24 litakuwa on kama masaa 10.
 
Wapo kibiashara zaidi kuliko kua ki huduma zaidi...umeme si anasa ni sawa na huduma ya maji! wizi ndio msingi wa nchi yetu
 

Ukiwa na fridge kubwa ndani ya nyumba fahamu kuwa matumizi yako kwa mwezi yatazidi units 75. Ila mtu km mimi ambaye cna fridge ndan ya nyumba nilishafanya calculation nikaona matumizi yangu kwa siku hayazidi units 2.3
 
Ukiwa na fridge kubwa ndani ya nyumba fahamu kuwa matumizi yako kwa mwezi yatazidi units 75. Ila mtu km mimi ambaye cna fridge ndan ya nyumba nilishafanya calculation nikaona matumizi yangu kwa siku hayazidi units 2.3

Bila fridge hesabu ni unit 1.79 kwa siku . Bulb tano ni za watt 40 kila moja jumla watt 200. Bila shaka matumizi ya unit 8 kwa siku bila fridge yanatia mashaka. Solution? Household survey ya kulinganisha bill na matumizi halisi.
 
Mi nilipogundua wananiibia sana na mi nimeamua kuwaibia mwaka sijui 8+ awajapata hela yangu siwezi kuwanufaisha CCM (Si munajua kuwa taasisi zote za serikali na majeshi yote umeme tunawalipia sisi na bado wenyewe hawakatiwi na hawana mgao)
 
Naaam hatuna budi kuifutilia mbali CCM kwanza Kama tunataka ustawi wa wananchi.... CCM ni adui wa haki na ustawi was jamii tuwakatae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…