Mnyalu Junior
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 573
- 200
Umeme ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya kila siku. Kwa Tanzania huduma hii inatolewa na kusimamiwa na TANESCO. Tunashukuru kwa huduma zinazotolewa na shirika hili. LAKINI kwa upande wa gharama ya matumizi ya nishati hii ndo kilio kwa Watanzania tulio wengi! Gharama ya Umeme ni KUBWA MNO, MNATUUMIZA!
Tunaomba muweke wazi tarrifs (makato) zenu! Mnadai mmetenganisha tarrifs za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa ambapo: Mtumiaji mdogo mmesema ni yule anayetumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 100 kwa unit; Na mtumiaji mkubwa mmesema ni yule anayetumia umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 350 kwa unit.
Nasema mnatuibia kwasababu; mbona mnatutoza gharama ya mtumiaji mkubwa ilihali baadhi yetu ni watumiaji wadogo? Kwa mfano MIMI mwenyewe toka nimeingiza umeme matumiz yangu kwa mwezi hayazidi unit 70 kwa mwezi na mnatoza gharama ya mtumiaji mkubwa! Na kibaya zaidi hamtozi Tsh350 kwa unit badala yake mnatoza 375 na point kadhaa! Acheni kutuibia bwana!
Nawasilisha wadau