TANESCO, kuna mgao?

TANESCO, kuna mgao?

Uko wapi mkuu? Huku Lushoto umekatika toka saa 11 isijekuwa issue kwenye grid ya taifa
 
Suala la ukatikaji wa umeme limekithiri sana siku hizi kama ndo mmeanza mgao mngetutangazia ili tujue na tujipange kuishi maisha ya kimgao kuliko hv mnavyofanya
Lakini kwa kanda ya ziwa wanajitahidi saana. Lazima tuwapongeze mkuu labuda leo tu usiku ndio giza. Mpaka sahiv.
 
songea ukatwaji wake ni tofauti kabisa wanakata washa kata washa yaani kama mtoto anachezea yaani songea inaboa hakuna mfano
 
Hata arusha wamekata tokea saa 11.
Jana walitangaz kupitia TBC kuwa watakata umeme kuanzia sa 2 asubuh mpaka 11 jioni kwa arusha......sasa nashangaa hata hiyo sa mbil bado lakn wameshaubeba..!
 
Niko msasani mkuu
Ila kutokana na coment za wengi inaonesha lilikuwa ni tatizo la sehemu kubwa ya Tanzania nasi walikata alfajiri hiyohiyo
 
Halafu juzi pia hatukuwa na umeme tangu asbh hadi 4:30 ucku
 
Itabidi JF wafungue jukwaa la tanesco maana matatizo ya umeme ni mengi sana
 
kuna msg inatembea whatsapp hii hapa labda itatoa mwangaza...

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mikoa waliounganishwa kwenye grid ya Taifa kuwa kimetokea tatizo la kiufundi kwenye GRIDI ya Taifa hivyo kupelekea wateja wetu kukosa umeme kuanzia majira ya saa 11:37 alfajiri.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Mafundi wanaendelea kufanyakazi ili kuhakikisha umeme unarejea mapema iwezekanavyo

MAENEO YANAYOATHIRIKA
Wateja wote waliounganishwa kwenye GRIDI ya Taifa.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:-
namba za kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100
Mitandao ya jamii www.facebook.com/tanescoyetu/ltd, www. twitter.com/tanescoyetu

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Imetolewa na:OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
 
Kuweni wa vumilia kuna maswala ya kiufundi tunayashughulikia...!
 
Back
Top Bottom