TANESCO Kigamboni kuna shida gani?

TANESCO Kigamboni kuna shida gani?

Nsubi_TheStar

Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
11
Reaction score
1
Habari wana forumn, mimi ni kati ya watu wengi waishio kigamboni wka sasa. Kinachonishangaza ni hali ya umeme kutokuwepo hasa wakati wa wikiendi. Utakuta jumamosi asubuhi umeme unakatika na hakuna hata taarifa ya nini kinaendelea. Siku nyingi za wiki umeme upo siku nzima ila ikifika wikiendi mambo yanabadilika.

Ni sawa inawezekana kuna hitilafu nk, ila basi hata taarifa!!! Hali hii inasikitisha sana.
 
Sio hilo tu...Kigamboni ukihitaji kuletewa Umeme ni shida

Yule meneja wa kigamboni anadai Rushwa waziwazi

Ukitaka nguzo moja zaidi ya kulipia gharama za kawaida unatakiwa kutoa Rushwa ya laki 2 na kuendelea

Kuna watu tumekaa miezi sita TANESCO hawataki kutuletea Umeme

Mbaya zaidi wanakata umeme wanavyotaka
 
Inatia hasira.....how comes umeme unakatika wikiendi tu...yani mpaka haieleweki sasa.
 
Sio hilo tu...Kigamboni ukihitaji kuletewa Umeme ni shida

Yule meneja wa kigamboni anadai Rushwa waziwazi

Ukitaka nguzo moja zaidi ya kulipia gharama za kawaida unatakiwa kutoa Rushwa ya laki 2 na kuendelea

Kuna watu tumekaa miezi sita TANESCO hawataki kutuletea Umeme

Mbaya zaidi wanakata umeme wanavyotaka

Huyo Meneja ni mzembe kabisa, watu tunataka umeme kuanzia huku Gezaulole, Mwongozo mpaka Dege lakini yeye anaangalia maslahi yake kwanza. Wengine tumeamua kutumia Solar ndio Tanesco yetu......unawaomba kama unataka umeme bure vile kumbe utaulipia na hapo ndipo wanapopata mishahara yao.....ili shirika linahitaji kusukwa upya kabisa...watu wanafanya kazi kwa mazoea mabaya....MASLAHI BINAFSI KWANZA!
 
Kaka bora wewe unaupata walau huo wa kukatika katika - sisi tulio maeneo ya pale kwa Mkorea - yule anayejenga chuo kikuu - maeneo ya pale hakuna hata dalili umeme utavutwa lini.

Nimefatilia Tanesco wanasema hawana Transfomer!! sasa sijui wanataka tuchange wananchi tununue la kwetu ndiyo waje kutufungia??

Siku hizi wala siendi tena, nimeamua kuishi kwa ka solar kangu ka taa tu -

Kuishi kigamboni kuna challenges nyingi - kuna muda huwa najilaumu bora ningeendelea kupanga Kijitonyama kuliko adhabu nayoipata kwa sasa.
 
Huku Kigamboni umeme unakatika mara 10 kwa siku, mnafanya mazoezi ya vitendo y kuwasha na kuzima umeme?
 
Sio hilo tu...Kigamboni ukihitaji kuletewa Umeme ni shida

Yule meneja wa kigamboni anadai Rushwa waziwazi

Ukitaka nguzo moja zaidi ya kulipia gharama za kawaida unatakiwa kutoa Rushwa ya laki 2 na kuendelea

Kuna watu tumekaa miezi sita TANESCO hawataki kutuletea Umeme

Mbaya zaidi wanakata umeme wanavyotaka

Una uthibitisho au unaongea tu kwa kuwa unamuda na bando ni lako? Kama ni kweli wanahitaji rushwa kwanini usichukue hatua stahiki?
 
Back
Top Bottom