Tamko: Ukweli uliojificha kuhusu Kitwanga kufukuzwa Uwaziri

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTANGULIZI
Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano huu mfupi ambao lengo lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha kuhusu kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari, taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa.

UFAFANUZI
Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais Dk John Pombe Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la kwamba Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa.

Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa sana na taarifa na uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika iliyopelekea Mhe Rais kufanya maamuzi haya. Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi ukilenga kumchonganisha Mbunge wetu na Mhe. Raisi uliopangwa na waovu wachache ambao wamebanwa na Serikali hii ya Awamu ya tano kupitia wizara hiyo nyeti kwa usalama wa nchi.

Itakumbukwa kuwa, Mhe Charles kitwanga alinadiwa na Mhe Rais na wanaCCM na baadae kupigiwa kura kwa wingi na wananchi wa Misungwi kwa ajili ya uwezo wake na dhamira yake njema ya kulinda taifa letu. Sisi wananchi wake, tunaamini katika uwexo wake, uadilifu wake na nidhamu ya kazi aliyonayo, hatuna mashaka na hili.

Baada ya kuteuliwa na Mhe Raisi kama Waziri wa mambo ya ndani, amekuwa muadilifu na kafanya mengi katika kuimarisha usalama na kufanya maamuzi yengi mazuri kwa maslahi ya taifa. Hili lilimtengenezea maadui wengi ndani ya serikali, ndani na nje ya CCM, mtandao wa dawa za kulevya, walioachishwa kazi NIDA na Uhamiaji. Watu hawa ndio waliochochea na kutengeneza mkakati wa kumchafua Mhe Kitwanga na walikuja dodoma kuhakikisha dhamira yao ovu inatimia.

USHAHIDI WETU
Miongoni mwetu tulikuwa mjini Dodoma pamoja na madiwani wa Jimbo la Misungwi ambao tulikwenda kumtembelea Mbunge wetu bungeni, tulizungumza mengi kwa ajli ya jimbo letu na katika kikao chetu hapakuwa na chembe ya kilevi chochote na hata kesho yake alipoinga bungeni alikuwa mzima wa afya ya kimwili na akili timamu na tunawahakikishieni kuwa Kitwanga hakuwa amelewa.

Ndugu waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 20 tulielekea bungeni kwa mwaliko wa Charles Kitwanga, tukiwa sehemu ya mualiko uliowajumuisha Madiwani wa jimbo lake tukiwa tumeambatana naye tukaingia ndani ya ukumbi wa bunge,tukashuhudia anajibu swali,baada ya kujibu swali la mbunge Sakaya,tulitoka nje na kupiga picha na madiwani wote wa Misungwi waliokuja kumtembelea Dodoma.

Baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika pale nje ya ukumbi wa Bunge, tulitoka na kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kututembeza maeneo yote ya Dodoma , lakini ilipofika jioni wakati tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa kuwa alionekana na Waziri Mkuu akiwa amelewa.

Ndugu wanahabari , tulishangazwa wote kwani tulikuwa tumekaa naye pale nyumbani kwake Dodoma (site 2) tukipata chakula cha usiku ,alionekana kutoaamini na hata madiwani pia na wengine ambao tulikuwepo hapa nyumbani kwake hatukuamini.

Tunachosema ni kwamba waziri Kitwanga hakulewa kama ambavyo imepotoshwa, bali alikuwa ni mkakati wa kumchafua na kuhakikisha andavuliwa wadhifa wake ili watu hawa waendelee kufanya maovu yao. Mtandao wa dawa za kulevya, pamoja na wale waliokuwa wanamshutumu kwamba amehusika kuondolewa kwao kazini wakiwemo Watu wa NIDA, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mfanyabiashara Said Lugumi pamoja na kundi mafisadi waliokwapua mabilioni ya fedha NSSF. Pia na baadhi ya wabunge wa CCM na Upinzani ambao walikuwa hawafurahishwi na kasi ya utendaji kazi wa Kitwanga katika Wizara ya Mambo ya ndani.

Kwa niaba ya wananchi wenzetu tunamuomba na kumtahadharisha Mhe. Rais awe makini na makundi la wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, pamoja na lile kundi la wanamtandao masalia ndani ya CCM na serikalini na kwenye vyombo nyeti vya ulinzi na usalama, ambayo kwa ujumla yalikuwa na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamtenganisha na kumpotosha Mhe Raisin a kumjaza habari zisizo za kweli.

Ndugu waandishi wa habari, kilichotushangaza zaidi baada tu ya Kitwanga kuvuliwa madaraka yake ya uwaziri, kuna watu walianza kufanya sherehe wakishangilia hususani wale waliovuliwa madaraka NIDA pamoja na NSSF,Uhamiaji na wale wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.

Ndugu waandishi wa habari, tunajua namna kundi la Said Lugumi, Ridhiwani Kikwete na kampuni yao walivyokuwa wanadhamini kwa mbinu za kifedha katika vita hii ya kitwanga ili aondolewe, lakini baada ya kuondolewa, wakajifanya kutoa taarifa ya kushangazwa kuondolewa kwake, Kitwanga amekuwa mtumishi wa serikali akiwa mtumishi mwandamizi benki kuu Tanzania (BOT),amekuwa mbunge na Naibu waziri kwa miaka 10,lakini hata siku moja hakuwahi kuonekana amelewa.

Ni muadilifu na ana nidhamu ya kazi, na nidhamu hii ndiyo iliyomfanya aaminiwe na kupewa dhamana hii.

MAAZIMIO YETU

=Tunaliomba Bunge kumuomba radhi Mhe. Charles Kitwanga kwa kumdharirisha mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Misungwi familia yake pamoja na watanzania wote waliokuwa wanaamini utendaji wake kupitia video iliyochezewa na wataalamu wa IT katika studio za Bunge ili kufanikisha lengo la kumuonyesha Kitwanga kuwa alikuwa amelewa bungeni.

=Tunamuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali bungeni atoe uthibitisho wa kikemia unaotanabaisha wazi kama Kitwanga alikuwa katumia kilevi wakati akiwa bungeni maana hakuna kipimo chochote kilichofanyika kudhibitisha uvumi huu.

=Tunaliomba Bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote walisambaza ile video inayoonyesha Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana amelewa wakati kiuhalisia hakulewa na alijibu maswali yote vizuri

=Tunaliomba Bunge kuchunguza idara ya habari ya Bunge pamoja na studio ile ya Bunge ambao wamehusika na kuhariri ile picha ya video iliyokuwa inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

=Tunahoji uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu ya ulevi bila uthibitisho wa daktari ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo kugundua kilevi cha mtu.

= Tunaomba Watanzania wote waliosikitishwa na taarifa hizi wajue tu kwamba ile video ambayo imemtia hatiani Kitwanga ilihaririwa kwa ustadi mkubwa kupitia wafanyakazi wa Bunge ambao wanapitia zile asadi za bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakupenda kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya kumhujumu na sasa wanasema kwenye vyombo vya habari ili kuhalalisha uhujumu huo.

=Tunaomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge wa Misungwi ambazo zinaonekana kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao kwani kisiasa zinaendelea kumchafua na kumharibia kwa wapigakura wake,familia yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .

=Tunajiandaa kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria kama watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Charles Kitwanga ambazo tunaamini zimetengenezwa kwa maslahi ya makundi yanayompinga ndani ya Serikali wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.

Pia tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini kundi la wanamtandao walio ndani ya serikali ambalo linaongozwa wahafidhina wasio taka mabadiliko ndani ya serikali .

Imeandaliwa na madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja na wakereketwa wa jimbo hilo.

Baraka Kingamkono,Gaudency Tungaraza na IDDY Majumuisho.

Asanteni na Mungu awabariki.

23/05/2016.
 
Dereva wa Kitwanga kahojiwa na NIPASHE kuhusu ulevi wa boss wake siku ile ya tukio kakiri kuwa jamaa alikuwa kalewa kweli.

Mbunge Ndassa naye kahojiwa kasema ni kweli jamaa yake na rafiki yake kipenzi alikuwa kalewa chakari siku hiyo ya tukio.

Sasa kama hawa watu wa karibu wamekiri kuwa jamaa kweli alikuwa kalewa, ina maana wameongopa??

Link hii hapa: Mawaziri 6 wamkwepa waziri aliyetumbuliwa
 
Raha ya Lumumba kila MTU ugombea maslai Yake ndio maana ni chama kinachoongozwa Na makundi sasa utaona waziri wakundi jingine atapigwa chini Vita ya lumumba ni maslai ya wenyewe kwa wenyewe naona sasa chz anamuona mchawi wake ni Riz
 
By Figganigga:

''...Itakumbukwa kuwa, Mhe Charles kitwanga alinadiwa na Mhe Rais na wanaCCM na baadae kupigiwa kura kwa wingi na wananchi wa Misungwi kwa ajili ya uwezo wake na dhamira yake njema ya kulinda taifa letu. Sisi wananchi wake, tunaamini katika uwexo wake, uadilifu wake na nidhamu ya kazi aliyonayo, hatuna mashaka na hili.........''

N.B Wakuu, Hii ni nukuu ya Figganigga toka taarifa Iliyoandaliwa na madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja na wakereketwa wa jimbo hilo kina Baraka Kingamkono, Gaudency Tungaraza na IDDY Majumuisho.

Published on 18 Oct 2015:

Dkt Magufuli amnadi Mgombea Ubunge Misungwi Ndg Kitwanga kwa maendeleo yakinifu wa wananchi wa Misungwi na Taifa zima la Tanzania.

Source: simu tv

Published on 21 May 2016
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani,Bw.Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kutenguliwa kwa kitwanga kumefuata taratibu za utumishi wa Umma.

Source: ITV TANZANIA
 
Mheshimiwa Charles Kiwanga ni vema ukakaa kimya badala ya kuagiza kundi la Madiwani wa Misungwi kuja Dar es salaam kukutea kwa waandishi wa habari kuwa uliwa haujalewa.

Leo kundi la Madiwani likiongozwa na Baraka Kingamkono, Gaudency Tungaraza na Iddy Majumuisho limefika jijini Dar es salaam na kutaka kupotosha umma kuwa Rais JPM alimwonea Kitwanga kutengua uteuzi wake kwani alikuwa hajalewa.

Nimesikitishwa na kitendo hicho cha madiwani kufanya Press conference na kutoa bahasha kwa waandishi waliofika ili wasaidie kupotosha jamii ili ione kuwa jamaa alionekwa kwa sababu ya kuwa na maadui wengi kama vile wauza dawa za kulevya, wafanyakazi wa NIDA walisimamishwa na kadhalika.

Madiwani hao wameenda mbali ya kumzushia Waziri Mkuu kuwa ndiye aliyemwona amelewa wakati Watanzania wote tulimwona kupitia TBC live wakati akishindwa kujibu swali la msingi la nyongeza.

Ni vema madiwani hao wakafanyakazi yao ni sio kuwa mawakili wa mlevi. Kama wao ni wakweli wangefanyia Press Conference Dodoma ili waandishi wa Dodoma waliokuwepo wawaulize maswali na wawajibu kwani ha kesi ulioifanyia Dodoma uendeshwa Dodoma iweje waje Dar kuna nini hapa na waandishi wa Dar.

Naomba PCCB mlifanyie kazi jambo hilo.

Kama madiwani hao wanatakuwaeleza ukweli Watanzania Mkutano huo wangeufanyia Dodoma ambapo tukio lilifanyikia badala ya kuwadanganya wananchi kupitia waandishi wa habari ambao hawakukuona siku ya tukio.

Sio kweli kitengo cha IT cha Bunge kilitengeza picha ili kukuchafua . Uchafu uliufanya mwenyewe.

Ndugu zangu waandishi wa habari hizo pesa mlizopesa na madiwani wa Misungwi ili kutetea uovu zitaipeleka nchi kubaya.

Mwisho CCM nawaomba muwachunguze Madiwani hao wanalo jambo. Ni vema ukabaki na wanachama wachache kuliko kuwa na wengi ambao wanasaliti chama.

Nawaomba waandishi wa habari sio kila kitu ni habari .

Mwisho.
 
Wana-Misungwi walimchagua Kitwanga kuwa Mbunge wao, period. Suala la Uwaziri ni la mamlaka ya Mteuzi. Kama wanataka wamuapishe wao kuwa waziri. Hizo zingine zoote ni porojo za kufurahisha barza.
Wana interest gani na Kitwanga? Aliwahidi nini? Make nashangaa haya matamko!! Hivi kwani kavuliwa ubunge?

Mimi nadhani hawa wanamatatizo ya kufikiri. Mie nadhani Kitwanga bado Mbunge wa Misungwi na kwa kupunguziwa majukumu, sasa anaweza kuwatumikia vizuri Wanamisungwi. Kwani Kitwanga alikuwa na ugomvi na Rais?

Au Waziri Mkuu? Mimi siamini kama wale waliomuona amelewa hawawezi kutofautisha mtu aliyekunywa na ambaye hajanywa.
 
Hizi ni pumba. yeye mwenyewe anahusika na lugumi.Ile video inaonyesha wazi kuwa alilewa ndio maana hata muuliza swali alisema duh waziri kaongea kwa mapozi.

Si hivyo tu angekuwa katika hali ya kawaida asingesema muuliza swali amesema kwa miaka mingapi kazi itakamilika kwani yeye anamiaka mingapi?.
 
napenda nitumie msemo wa 'what goes around comes around' kama kuna watu wamemchafua Kitwanga ili aondolewe kwenye uwaziri, watakuja kupata malipo yao.
 
Nchi imepoteza mwelekeo hii, tatizo viwavi wamekuwa wengi mno. kwa maana hiyo wanataka Rais atoe uthibitisho wa kilevi cha kitwanga? wao kama nani? hawajui kwamba kitwanga katimuliwa kwa public interests?
 
Back
Top Bottom