Tamko la mtandao wa IPTL bring back our money (ibbom)

Tamko la mtandao wa IPTL bring back our money (ibbom)

chuuma

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2015
Posts
363
Reaction score
557
TAMKO LA MTANDAO WA IPTL BRING BACK OUR MONEY (IBBOM)
UTANGULIZI.

Ndugu waandishi WA habari awali ya yote tuanze kwa kumshukuru Mungu kwanza kwa kutukutanisha tukiwa salama. PILI tuwashukuru ninyi watanzania wenzetu kwa kukubali kuitikia wito wetu na kujumuika nasi siku hii ya Leo na ya kihistoria katika maisha yetu na kwa watanzania wote kwa ujumla wao.

Tulianzisha kundi hili kwa kukumbuka historia ya wa Nigeria ambao mabinti wao walitekwa na Bokoharamu na hivyo wakaanzisha kampeni za BRING BACK OUR GIRLS(BBG) nasi kwa kutambua umuhimu wa kupigania rasilimali za nchi yetu tukaanzisha kundi la IPTL BRING BACK OUR MONEY (IBBOM)

Sisi Bokoharamu wetu ni watala mafisadi na hivyo tunawataka warudishe fedha zetu,na ndio msingi wa kampeni yetu endelevu na ya kudumu ya IPTL-BRING BACK OUR MONEY.

Ndugu waandishi wa habari mtakumbuka ni takribani mwaka mmoja umepita tangu tulipokutana nanyi katika ukumbi wa Travertine hotel pale magomeni wakati huo tulikuwa katika hali hasira kwani tulikuwa katika mapambano makali dhidi ya ufisadi na mafisadi waliokwapua fedha zetu katika akaunti ya TEGEGA ESCROW kiasi 306 bilioni ambazo licha ya watuhumiwa wake kufahamika lakini mpaka sasa pesa hazijarudishwa japo baadhi wamefikishwa mahakamani lakini baadhi yao bado hawajafikiahwa kortini.

Ndugu waandishi wa habari tumewaita hapa Leo kwa lengo kubwa LA kumpongeza na kumshukuru mh. David Kafulila (MB) kwa ujasiri wake na uzalendo wake wa kuamua kupambana na mafisadi na ufisadi mpaka kufikia hatua ya sasa kwani amepitia mengi katika hatua yake ya kupambana na jambo hili ikiwemo vitisho na kejeli nyingi mpaka kupelekewa kuita "TUMBILI"

Ndugu waandishi wa habari mtakumbuka pia mh. KAFULILA alianza vita hii akiwa mnyonge na mpweke lakini katika ya safari hiyo ngumu yenye miiba hakukata tamaa, hats hivyo katika ya safari sisi watanzania wazalendo tulijitokeza na kumuunga mkono Mara baada ya kukaa naye na kujifunza mini hasa escrow na yaliyomo ndani yake, ndipo tulipogundua kulikuwa na HOJA ya msingi ya kuisimamia na kuisema kwa nguvu kwani ilikuwa na maslahi kwa watanzania ndipo tulipoamua kuungana naye ikiwemo kuiomba mahakama kuishitakiwa naye ingawa hatukukubaliwa.

KWANINI TUMEWAITA?

Ndugu waandishi wa habari tumewaita hapa Leo kwaajili ya kuiambia Tanzania na watanzania kwa ujumla kuwa nchi yetu inahitaji kuwa na wabunge aina ya KAFULILA hivyo basi,

Mosi, tunawapongeza wananchi wa kigoma kusini kwa kumpata mbunge mwenye kuelewa na kuwa na uwezo kuwasilisha mawazo yao, lakini kubwa zaidi kuwatetea kwa nguvu bila woga.

PILI, kuwaomba tena wananchi wa kigoma kusini kumchagua tena mh. KAFULILA ili aendelee kutetea maslahi ya Taifa

Tatu, Sisi kama watanzania wazalendo na bila kujali itikadi zetu ila mapenzi kwa Taifa letu, tumechangishana shilingi mia, mia tano nk na tumefanikiwa kupata kiasi cha fedha Tsh 5Milion cha kumtosha kwenda kuchukulia fomu na hivyool basi tutamkabidhi ili iwe sadaka yetu na maombi yetu kwake ili arudi tena bunge la 11.

SHUKURANI.
Tunatoa pongezi kwa kituo cha watetezi wa Haki za binadamu (Human Rights Defenders) kwa kumpa tuzo kama alama ya ujasiri na uzalendo kwa taifa lake.Lakini pia tunapongeza taasisi hiyo na ile ya Legal and Human Rights Centre (LHRC) kwa pamoja kwa kuendelea kumsaidia msaada wa kisheria na uwakili mahakama kuu ya Tanzania katika kesi ambayo anashitakiwa na kampuni ya IPTL ,PAP ,na Harbinder Singh Sethi eti aliwachafua na hivyo awalipe zaidi ya 3000bilion.

PILI tunawapongeza sana wananchi wa wilaya ya kahama mkoani shinyanga kwa kuamua kumsimika kuwa chifu WA kabila lao na kwa hakika hayo yalikuwa maombi kwake hivyo ni ishara kuwa jamii nzima ya watanzania inaunga mkono jitihada zake za kuwatetea watanzania.

Tatu lakini kwa umuhimu mkubwa ni kuwashukuru watanzania kwa ujumla wao hususuani ni wale wanamtandao huu wa wazalendo na watetezi wa watanzania wanyonge, lakini pia shukurunai za pekee kwenu nyie wanahabari kwa kushikamana nasi katika kipindi chore cha mapambano haya.

HITIMISHO.

Ndugu wanahabari katika kuhitimisha tunaomba kuendelea kusisitiza kuwa agenda ya ufasadi na mafisadi ni yetu site hivyo basis ni vema tukashirikiana ili pia ukweli kuhusu suala la mabehewa feki yaliyoligharimu taiga kiasi Tsh 238bn,ufahamike kwa ufasaha kwa watanzania .Tumedhamiria kulifuatilia kwa kina hili suala na tutakapojiridhisha juu ya ufisadi huu tutaanzisha vuguvugu kubwa nchi nzima kama njia ya kutetea rasilimali zetu zinazoliwa na walafi wachache huku Huduma za jamii zikidolola kwa kiasi kikubwa.

SEMA UFISADI SASA BAASI TUMECHOKA.

Kwa niaba ya wanakundi wa IBBOM,
Baraka Mfilinge
 
Asante kwa kumpa zawadi mr kafulila,lakin mbona sisi hatukuchangia hizo hela.
Lakin pia KICHWA CHA HABARI KINAONGELEA TAMKO,LAKIN MIM CJALIONA TAMKO HAPO au je!?
 
Asante kwa kumpa zawadi mr kafulila,lakin mbona sisi hatukuchangia hizo hela.
Lakin pia KICHWA CHA HABARI KINAONGELEA TAMKO,LAKIN MIM CJALIONA TAMKO HAPO au je!?

Kwani na ww ni mmoja wa hao waliokuwepo ktk mtandao huo
 
Wanigeria walipoanzisha kampeni ya BRING BACKS OUR GIRLS (BBOG) walikuwa wanafahamu waliowateka/wanaowashikiria wasichana wao.

Watekaji hao walikuwa Boko Haram. hivyo Wanigeria walikuwa wanawaambia Boko Haram BBOG

Nyinyi pia mmeanzisha kampeni ya IPTL BRING BACKS OUR MONEY (IBBOM). Lakini tofauti na BBOG, nyinyi hamuwataji kwa majina hao wanaotakiwa kurudisha pesa zetu.

Ili kampeni hii iweze kuwa successful, kwanza inabidi tuwafahamu kwa majina hao tunaotaka waturudishie pesa yetu.

Then tukishawafahamu kwa majina ndiyo tuwaambie kwamba wanatakiwa kuturudishia hizo pesa zetu.

Kuanzisha IBBOM, bila kuwafahamu hao wanaotakiwa kurudisha hiyo pesa, it is like shooting around the bush not shooting the enemy.

The ball is in your court, we need to know them first.
 
Acha makongoro aingie ikulu akawanyooshe hao vibaka
 
Acha makongoro aingie ikulu akawanyooshe hao vibaka

Mkuu shuma50, hata mimi mwanzo niliwaza kama wewe kuwa Makongoro ndio mwarobaini wa "vibaka", lakini siku zinavyoendelea na kuona kwake "kibaka" ni Lowassa tu, na sisikii akiongelea vibaka wa escrow, epa, rada nk nimeanza kumwona kuwa na yeye ni wale wale tu! Hana jipya!
 
Amna endelea kumwamini tu Makongoro Nyerere alisema vibaka sio kibaka...sema amekomaa na uyo cz ndio anaonekana kuikamia zaidi ikulu na anatumia nguvu kubwa sana plus media support ...makongoro the young master mzalendo halisi
 
Wanigeria walipoanzisha kampeni ya BRING BACKS OUR GIRLS (BBOG) walikuwa wanafahamu waliowateka/wanaowashikiria wasichana wao.

Watekaji hao walikuwa Boko Haram. hivyo Wanigeria walikuwa wanawaambia Boko Haram BBOG

Nyinyi pia mmeanzisha kampeni ya IPTL BRING BACKS OUR MONEY (IBBOM). Lakini tofauti na BBOG, nyinyi hamuwataji kwa majina hao wanaotakiwa kurudisha pesa zetu.

Ili kampeni hii iweze kuwa successful, kwanza inabidi tuwafahamu kwa majina hao tunaotaka waturudishie pesa yetu.

Then tukishawafahamu kwa majina ndiyo tuwaambie kwamba wanatakiwa kuturudishia hizo pesa zetu.

Kuanzisha IBBOM, bila kuwafahamu hao wanaotakiwa kurudisha hiyo pesa, it is like shooting around the bush not shooting the enemy.

The ball is in your court, we need to know them first.

Mkuu Bobuk, you have a big point here! Huu mtandao ungaliwataja japo kwa majina hao wanaotakiwa kurudisha hizo fedha wangalikuwa wameshashinda karibu nusu ya vita wanayotaka kupigana! Hiyo nusu nyingine wangeweza kuwaachia wananchi na wadau wengine na uhakika wa ushindi i.e fedha kurudishwa kweli, ingekuwa ni uhakika wa 100%. Nje ya hapo hao jamaa wanatafuta "publicity" tu!
 
Hongera mh kafulila,kiboko ya mafisadi na mwakani watakukoma ongeza speed ukiwa wizara ya fedha kama waziri kupitia ukawa
 
Ni hatua nzuri lakin hiyo ni punje ndogo tu ya hela zilizoibwa hapa nchini. Hela zilizofisidiwa ni nyingi sana. Tungeanzisha kampeni ya kudai zote
 
BBOM - bring back our money ndio ilikuwa iwe kampeni yetu wote. Mtu fisadi akitangaza nia tunabeba mabango yaliyoandikwa BBOM. RUdisha fedha zetu kwanza - RUFEZEKWA
 
Wanigeria walipoanzisha kampeni ya BRING BACKS OUR GIRLS (BBOG) walikuwa wanafahamu waliowateka/wanaowashikiria wasichana wao.

Watekaji hao walikuwa Boko Haram. hivyo Wanigeria walikuwa wanawaambia Boko Haram BBOG

Nyinyi pia mmeanzisha kampeni ya IPTL BRING BACKS OUR MONEY (IBBOM). Lakini tofauti na BBOG, nyinyi hamuwataji kwa majina hao wanaotakiwa kurudisha pesa zetu.

Ili kampeni hii iweze kuwa successful, kwanza inabidi tuwafahamu kwa majina hao tunaotaka waturudishie pesa yetu.

Then tukishawafahamu kwa majina ndiyo tuwaambie kwamba wanatakiwa kuturudishia hizo pesa zetu.

Kuanzisha IBBOM, bila kuwafahamu hao wanaotakiwa kurudisha hiyo pesa, it is like shooting around the bush not shooting the enemy.

The ball is in your court, we need to know them first.

ni Kampuni ya IPTL kaka au unawataka akina nani tens
 
BBOM - bring back our money ndio ilikuwa iwe kampeni yetu wote. Mtu fisadi akitangaza nia tunabeba mabango yaliyoandikwa BBOM. RUdisha fedha zetu kwanza - RUFEZEKWA

Wakati wake bado kaka ,hii ni wakati wa kampeni inabidi T-Shirts zitengenezwe kwa wingi ili wakija kwenye kampeni wagombea wote wa CCM inabidi tuwavalie kuwakumbusha tu warudishe pesa zetu kwanza ndiyo wapande jukwaani kujinadi.Kuanzia na nafasi ya URAIS mpaka udiwani......

Hiyo inatakiwa iwe slogan ya mwaka huu.
 
Hakika Getty
 
Kama Kichwa cha habari haiendani na main body , basi haina Mantiki ila tumekuelewa mkuu.
Mafisadi basi
 
Back
Top Bottom