Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
SIKU chache baada ya kundi lililojiita Madiwani wa Jimbo la Misungwi kutoa tamko la kumtetea Charles Kitwanga, tamko hilo limeelezwa kuwa feki.
Tamko hilo lilitolewa kupinga hatua ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa Kitwanga, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Uamuzi huo ulifanywa tarehe 20 Mei mwaka huu.
Antony Bahebe, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi amesema kuwa, madiwani waliojitokeza kumtetea Kitwanga ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, halina baraka za madiwani wa halmashauri hiyo kwa kuwa, hawajawahi kukutana katika kikao chochote na kuazimia kutoa tamko hilo.
Kundi hilo la madiwani ‘feki’ lilitoa tamko rasmi kwa vyombo vya habari likimtetea Kitwanga ambaye alidaiwa kuingia bungeni na kujibu maswali yaliyohusu wizara yake akiwa amelewa.
Katika tamko lao, kundi hilo la madiwani ‘feki’ lilieleza kushangazwa na kutoridhishwa kwao na uamuzi wa Rais Magufuli wa kumvua uwaziri Kitwanga kwa kile kilichodaiwa na kundi hilo kuwa, hakukuwa na uthibitisho wa kitabibu kuhusu tuhuma za ulevi wake (Kitwanga).
Madiwani hao ‘feki’ walidai, walikuwa nyumbani kwa Kitwanga mkoani Dodoma baada ya kupewa mwaliko na mbunge wao.
“Tulitoka na kuelekea katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kututembeza maeneo yote ya Dodoma, lakini ilifika jioni wakati tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa kuwa, alionekana akiwa amelewa,” ilieleza sahemu ya taarifa yao.
Kundi hilo lilidai kuwapo kwa kundi la wafanyabiashara wa dawa za kulevya, mafisadi wakiwemo maadui wa Kitwanga na makundi ndani ya CCM kuwa ndio waliotoa taarifa za uongo kwa Rais Magufuli na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu kwa maslahi yao binafsi.
Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri hiyo (Bahebe) ameueleza mtandao huu, “ni kwamba sisi madiwani wa Misungwi hatujafanya kikao cha aina yoyote ikiwemo kutoa tamko la kupinga kutenguliwa kwa mbunge wetu katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani.
“Tunaamini Magufuli ndiye aliyemteua na ndiye aliyetengua uteuzi huo. Je, sisi tuna nguvu gani ya kupinga maamuzi ya mkuu wa nchi?” amesema mwenyekiti huyo.
Mtandao huu umemtafuta Kitwanga ili kuzungumzia tuhuma za kuunda kundi la madiwani kwa ajili ya kumsafisha katika jamii.
“Naombeni jamani mniache mimi nimechoka na maneno! Watu wameongea mengi, mimi sitaki maneno sijui chochote niacheni nipumzike,” amesema Kitwanga.
Mmoja wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye hakupenda kuandikwa jina lake liandikwe ameeleza kushangazwa na nguvu ya kundi hilo la madiwani kulitaka Bunge na Serikali kutoa ushahidi wa kikemia unaoonesha ulevi wa Kitwanga.
“Hivi hawa watu waliojitwisha uwakilishi wa wana Misungwi wamepata wapi mamlaka ya kupingana na rais ambaye ndiye alimteua bila ushawishi?
“Leo hii amemvua uteule alalamikiwe na kundi dogo kama hilo? Mawaziri wangapi walishatenguliwa mbona hatukuona kundi likijibatiza kuwa ni Madiwani?”