TAMISEMI ni kweli wasitisha uhamisho

TAMISEMI ni kweli wasitisha uhamisho

mtei msomi

Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
16
Reaction score
4
Wadau naomba mnisaidie eti tamisemi wamesitisha uhamisho mfano wa kubadilishana hadi uhakik wa watumshi hewa ukamilike au bado uko palepale,mwenye taarfa anisaidie mana hapa nimeshaathirika kisaikolojia mana hata kazi nafanya tu kwasababu napata mshaara lkn sins mnkari na kazi kabisa kwani fikra zangu zilishahama kabisa.nisaidieni taarifa wadau ili njiandae kisaikolojia mana karibia vitu vyote nimeshauza
 
1471025584946.jpg
huyu mwingine alitaka kula laki tano yangu kiulaini tu...Tapeli mkubwa!Hope vyombo husika vitamfuatilia na kumtia nguvuni.
 
tamisemi wamepiga sana hela za watumishi wa uma...

wametajirika sana dodoma kwa style ya kusaidia watu kuhama vituo
 
Subiri mpaka watakapo tangaza tena,maana hata ajira,kupandisha vyeo vimesitishwa.Wapo Walimu waliograduate 2015 wanakutana na wenzao wa 2016 kitaaaani
 
Msihame fanyeni kazi kwa uzalendo vijana, mnataka kwenda wapi Tanzania yetu sote!
 
Pole sana mkuu..unanikumbusha kipindi naangaikia uhamisho wangu...ni wakat mgumu sana...psychologically and physically
 
Msihame fanyeni kazi kwa uzalendo vijana, mnataka kwenda wapi Tanzania yetu sote!
Kufuata mke wako au mume wako kama wote ni watumish wa umma vinginevyo ni chanzo cha uzinzi na maambukiz na watoto wa kuzingiziwa na nadhan hiyo ndiyo sababu kuu. Na zinginezo zipo
 
Uhamisho wa kubadirishana vituo vya kazi ndio mzuri zaid kwa maana hauachi uhaba wa watumish mahali pengine hata mimi naunga mkono uhamisho wa aina hii 100% ingawa sina hakika na ufanisi wake
 
Kufuata mke wako au mume wako kama wote ni watumish wa umma vinginevyo ni chanzo cha uzinzi na maambukiz na watoto wa kuzingiziwa na nadhan hiyo ndiyo sababu kuu. Na zinginezo zipo

Kwa hiyo kama mke anahamahama na wewe utamfuata kama kumbikumbi acheni hizo sasa kila mtu akimfuata mke wake au mume wake nani atabaki kituoni kufanya kazi,uwe na sababu za msingi kama vile ugonjwa unafuata matibabu lakini hii ya mke/mume iko very light
 
Hiyo barua hata waliolazwa Mirembe ukiwapelekea hyo kitu haraka watakwambia ni feki.....
 
Kwa hiyo kama mke anahamahama na wewe utamfuata kama kumbikumbi acheni hizo sasa kila mtu akimfuata mke wake au mume wake nani atabaki kituoni kufanya kazi,uwe na sababu za msingi kama vile ugonjwa unafuata matibabu lakini hii ya mke/mume iko very light
Hivi wewe ni mtu mzima au mtoto maana naweza nikawa napoteza mda wangu humu bila sababu ,kama hata maana ya ndoa huijui !? Au ndo kile kikosi cha O-Level kilicho vamia jukwaa.
 
wafanyakazi wa serikalini ukiondoa level za management.. wengi wao ni maskini.. sababu wanapenda sana kulalamika lalamika na excuses...

kazi za private hazinaga mambo ya kumfata mume sijui mke na watu hawalalamiki lalamiki..

kazi sio baba yako... ukiona anakuweka mazingira ambayo hutaki kuishi unaacha na kutafuta nyingine kama upo competent huwezi shindwa kupata au kufanikiwa kwa miradi yako.. tanzania bado virgin sana..

ushawai kuona mtanzania mwenye asili ya india, mwarabu au mzanzibar kaajiriwa halmashauri sitimbi??

anaona mizinguo tu ndio maana anaamua kushinda dukani kwake mijini tu... na bado anaishi maisha mazuri kuliko watumishi wengi.. gari nzuri, watoto wake wanasoma shule nzuri... sabab anatumia akili yake vizuri....
 
Acha uongo na unafiki kila taasisi iwe ya umma au private ina fahamu umuhimu wa hilo kinacho kuwa kigumu ni kwamba taasisi binasi inaweza ikawa sehemu moja tu na hivyo huwez kuhama kwa mfano unafanya kazi geita gold mining utaomba uhamie kwenye mgodi gani hapa ambao nao upo chini ya geita lakin upo dar es salaam?? Ika kama mpo taasisi moja na ni mke na mume sekta binafsi zina litambua hilo kuwa lipo na inalitekeleza sababu ni sheria na sheria katika nchi inatawala kote sekta binafsi na serikali kwa ujumla, usitumie majibu mepesi kujibu maswali magumu.
 
Kwa hiyo kama mke anahamahama na wewe utamfuata kama kumbikumbi acheni hizo sasa kila mtu akimfuata mke wake au mume wake nani atabaki kituoni kufanya kazi,uwe na sababu za msingi kama vile ugonjwa unafuata matibabu lakini hii ya mke/mume iko very light
Kama huna ndoa nyamaza
 
Umeolewa??
 
Back
Top Bottom