Wakati viongozi, wafanyabiashara na makampuni makubwa barani Afrika yakitajwa kwenye kashfa ya ukwepaji kodi ya Panama Papers, TAKUKURU imesema inafuatilia ripoti hiyo kubaini kama kuna Watanzania waliohusika.
Kashfa hiyo inayoendelea kutikisa dunia inahusisha nyaraka zilizoibuliwa na mtandao wa waandishi wa habari ambazo zinawafichua watu maarufu duniani, wakiwamo wakuu wa nchi 12 walioko madarakani na waliostaafu pamoja na familia na rafiki zao wa karibu ambao wamenufaika na ukwepaji kodi.
Wakati nchi za watu maarufu kutoka nchi za Afrika kama Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Zimbabwe, Angola, Congo na Rwanda zikitajwa kwenye kashfa hiyo, hakuna Mtanzania wala kampuni ya hapa nchini iliyohusishwa.
Lakini mkurugenzi wa TAKUKURU,Kamishna Valentino Mlowola aliiambia Mwananchi kuwa taasisi yake bado inafuatilia kashfa hiyo ili kujua kama kuna Watanzania wanahusika.
Alisema endapo itabainika kuwapo kwa Watanzania kwenye kashfa hiyo, watachukuliwa hatua kulingana na sheria zilizopo.
“Ninachoweza kusema kwa sasa tunaendelea kuangalia ripoti na tukibaini uwepo wa Watanzania, mambo mengine yatafuata ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kulingana na sheria zetu,” alisema Mlowola.
Mkuu wa Polisi wa Kimataifa (Interpol), Gustavus Babile alisema kitengo chake kitaingilia kati sakata hilo endapo kutakuwa na ulazima baada ya kugundua jinai.
“Mpaka sasa hakuna lolote tunalofanya kuhusu kashfa hiyo ila tunaweza kuingia endapo atahusika Mtanzania na itakapoonekana kuna kosa la jinai linalomhusisha mtu wetu,” alisema Babile.
“Zipo mamlaka nyingi nchini ambazo zinaweza kufuatilia sakata hili. Interpol itaingia pale tutakapoona kuna ulazima.”
Lakini Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage alisema wizara yake haihusiki na kashfa hiyo, akieleza kuwa inayohusika ni Wizara ya Fedha na ya Katiba na Sheria, akitaka mwandishi awasiliane na wahusika kwenye wizara hizo.
Hata hivyo, nyaraka za Panama zinamtaja mfanyabiashara maarufu barani Afrika, Aliko Dangote, ambaye anamiliki kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara nchini.
Akizungumzia sakata hilo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magreth Sakaya alisema hatashangazwa endapo Watanzania watatajwa kwenye kashfa hiyo.
Alisema nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikisumbuliwa na jinamizi la ulafi na ubinafsi wa viongozi, huku wengi wao wakijali matumbo yao na familia zao.
“Tukiangalia tulikotoka na viongozi tuliokuwa nao, nchi ilikosa usimamizi hali iliyosababisha ufisadi kushika kasi, kila mmoja alijilimbikizia fedha alivyoweza,” alisema mbunge huyo Kaliua.
“Hata ukiangalia mijadala yetu bungeni, iligusia suala la watu kuficha fedha nje. Pia vitega uchumi vingi vinamilikiwa na vigogo na familia zao.”
Sakaya alisema kuna haja ya uchunguzi wa kina kufanyika ili kuangalia uwezekano wa vigogo wa Tanzania kuwepo kwenye sakata hilo.
Kuanikwa kwa nyaraka hizo ni matokeo ya kazi iliyofanywa na kampuni ya Mosack Fonseca inayojihusisha na utoaji wa huduma za kisheria hasa kodi kwa taasisi na kampuni za kimataifa.
Shughuli kubwa ya kampuni hiyo yenye makao yake makuu Panama City, ni kuratibu matumizi sahihi ya misamaha ya kodi inayotolewa na mataifa tofauti duniani.
Miongoni mwa vigogo waliotajwa ni Rais wa Russia, Vladimir Putin, ambaye anadaiwa kuficha Dola 2 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh4 trilioni) kwa kumtumia swahiba wake, Sergei Roldugin, ambaye ni mwanamuziki.
Wengine ni baba wa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, hayati Ian Cameron, wabunge sita kutoka Bunge la (House of Lords), watatu wa chama cha Consevertive na wafadhili wa vyama vya siasa vya taifa hilo inaelezwa wana mali nje ya nchi ambazo hazilipiwi kodi.
Nyaraka za Panama zimewataja pia shemeji yake Rais wa China, Xi Jinping; Rais wa Argentina, Mauricio Macri; na watoto watatu kati ya wanne wa Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif; Waziri mkuu wa mpito wa taifa hilo, Ayad Allawi pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Iraq.
Kwa Afrika waliotajwa mpaka sasa ni Rais wa zamani wa Sudan, Ahmad Ali al-Mirghani; Naibu Jaji Mkuu wa Kenya, Kalpana Rawal; na Kojo Annan, mtoto wa aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan.
Inadaiwa watu hao walitumia kampuni hewa kununua nyumba katika mitaa ya kifahari jijini London, Uingereza ikiwa ni mbinu ya kutakatisha fedha.
Chanzo: Mwananchi