Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,297
- 18,046
Taifa Stars tatizo ni Kim Poulsen?
Taifa Stars imetolewa na tayari wadau wanatoa sababu mbalimbali hasa ikizingatiwa katika siku za karibuni ilionekana kufanya vema kwenye mechi za kujipima nguvu dhidi ya Zambia na Cameron. Moja ya sababu ambayo imeandikwa kwenye gazeti la Mwananchi ni wachezaji kutojituma. Wametajwa akina Chuji, Bocco na Sure Boy. Kama hayo yanayoelezwa ni ya kweli basi huenda kocha wa timu yetu, Kim Poulsen ana matatizo ya Man Management Tofauti za siku za nyuma wakati wa FAT ya akina Ndolanga, sote tunajua wachezaji hawakuwa na motisha ya kuchezea timu ya taifa, labda kwa ajili ya uzalendo tu. Viongozi pia walichangia sana kwa kutoa vitisho na kuwapiga maarufu baadhi ya wachezaji kuchezea timu ya taifa. Ilikuwa kama timu binafsi ya Ndolanga. Sasa wakati huu kuna wadhamini wa uhakika na kambi za maandalizi za kiwango kizuri, kwa nini wachezaji wasitake kuchezea timu ya taifa?. Angalau Chuji alieleza sababu za msingi maana alijiona ni mtu wa kukamilisha namba tu lakini hakuwa na matumaini ya kucheza. Hali kama hii ilimtokea Michael Carrick wa Uingereza akaamua kujitoa japo sasa karejea baada ya kuhakikishiwa uwezekano wa kucheza. Sababu za Sure Boy na Bocco bado ni kitendawili . Yote hayo yanaashiria kuna walakini katika namna Kim Poulsen anavyohusiana na wachezaji (Man management). Imefika mahali wengine wanajiona hawana thamani kwenye timu na hilo ni kosa kubwa sana kwa kocha. Mwalimu lazima awe na uwezo wa kuwaweka sawa hata wale wasiopata namba ili wajione ni sehemu ya timu. Ndiyo moja ya siri ya mzee Alex Ferguson. Inaelekea Kim Poulsen tayari ana kuwa na watu wake hata kama wengine watafanya bidii ya namna gani ni kazi bure tu. Tunajua alikuwa na malengo hasa ya kuwandaa vijana kwa siku za usoni, lakini ili kupita vigingi kwa wakati huu alihitaji sana kutumia uzoefu wa akina Chuji kuelekea huko. Mchezaji akiona hayumo katika hesabu za mwalimu zaidi ya kukamilisha namba, matokeo yake ndiyo hayo tuliyopata dhidi ya Uganda. Kwa jinsi hali ilivyo, tuna njia mbili tu. Ama Poulsen abadilike na aambiwe kabisa na viongozi wa TFF, au kama hilo litakuwa gumu kwake, aachie ngazi aje mwalimu mwingine. Kama Poulsen ataondoka, ni vyema tukatumia kocha mzalendo wakati tunatafakari mustakabali wa siku za usoni. Akina Marsh lazima waendelee katika bench la ufundi ili kuwe na mwendelezo. Nawasiliasha