sajenti umeongea mengi na kwa uchungu sana. Ndiyo maana ukitazama utaona thread yangu,''tatizo la Taifa Stars ni kocha?''nami nakukaribisha kuchangia. Mimi nafikiri kwa jinsi tunavyoendesha soka letu na michezo yote kwa ujtmla,ni kama uwe Ulaya halafu usiku umeme ukatike ghafla.Kibiriti hujui uanzie kukitafutia wapi! Pamoja na udhamini mkubwa,makocha wa kigeni,wachezaji tulio nao,hatufiki mbali kimichezo,hususan soka,achilia mbali kuchukua vikombe. Huwa naangalia mataifa kama Chezc Republic,Uholanzi na Ugiriki. Kwa muda mrefu hawakuwa wamechukua vikombe lakini WAMO KWENYE RAMANI YA SOKA! Kuwa kwenye ramani ya soka kunaleta matarajio ya kuchukua vikombe hapo mbeleni.. Tufanyeje? Tafakari.. Pitia thread yangu uangalie.