Taifa lipo ila watu wanapita

Taifa lipo ila watu wanapita

kelebhe

Member
Joined
Jan 25, 2020
Posts
41
Reaction score
39
Anachokufanya Mbunge wa Hai Mheshimiwa Mbowe kuomba maridhiano kabla ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni jambo la msingi sana. Ni suala ambalo linatakiwa kuchukuliwa kama ukomavu wa kifikra na sio udhaifu katika uongozi.

Mbowe ameangalia mbali sana kwa sababu anachokiangalia ni taifa kwanza na siyo binadamu maana sisi tunapita lakini taifa litaendelea kuwepo, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha ya kwamba tunalikinda taifa hili kwa gharama yeyote ili vizazi vinavyokuja navyo vifurahie taifa lao kama ilivyo kwa kizazi hiki.

Hata vitabu vya dini vimeweka wazi faida zitokanazo na maridhiano kuliko kutumia njia ambayo inaweza kuhatarisha mstakabali wa amani.

Wahusika wote katika hili kaeni pamoja muone namna ambavyo mnaweza kufanya ili kuondoa hii minong'ono ambayo inaazpnza kujitokeza kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Chochote kikitokea itakuwa ni pigo kwetu sisi Kama taifa kwa sababu tulishahaminisha mataifa huko duniani ya kwamba taifa letu ni la amani na kwamba tutafanya jitihada zote kuilinda amani yetu.

Hivyo naunga mkono njia ya maridhiano kama ambavyo anaomba Mbowe kulinda amani ya taifa letu.
 
Back
Top Bottom