MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 15,597
- 39,374
Wanafki na wenye husda hawasikii noah wala makinikiaHaya yote yataisha bomberdier na Noah zetu zikifika.
Tutakuwa tunasafirisha makinikia yetu wenyewe
upuuzi ni tabia ya kupuuzia mambo mimi nafikiri tunasifa mbaya zaidi ya hiyoSiamini kama kuwa watu wapuuzi duniani Zaidi ya watanzania.
hiyo ni shida kubwa sana ya jamii yetu, mambo mengi mabaya yamekua yakifanyika na watu wamekua wakiyashangilia na nchi inaendelea kuwa masikini kila sikuMi huwa nachoka sana kumpapalikia mtu kinafiki hta kama anahela
Husda ni roho ya chuki imwingiayo mtu anapopata taarifa kuwa mwenzake amepata au amefanikiwa, roho hii inamfanya asiwe na furaha na atatafuta namna ili mwenzake aharibikiwe. Hii ni ile roho ya mtu kutopenda watu wengine wawe na mafanikio, kutaka watu waishi maisha ya shida, wawe wanataabika.husda maana yake ni nini mkuu.
hizo ni tabia za watu weusi wenye asili ya afrika popote walipo duniani.
nashukuru sana mkuu nimeelewa sana.Husda ni roho ya chuki imwingiayo mtu anapopata taarifa kuwa mwenzake amepata au amefanikiwa, roho hii inamfanya asiwe na furaha nakutafuta namna ili mwenzake aharibikiwe. ile roho ya mtu kutopenda watu wengine wawe na mafanikio, kutaka watu waishi maisha ya shida, wawe wanataabika.
Haya ni matatizo ambayo lazima mkakati wa kitaifa uundewe ili kuyaondoa, ni mambo ya kishamba na kizamani sana, mataifa yalioyoendelea vitu hivi havipo kwa kiwango cha hapa kwetuWatanzania tumebarikiwa chuki, roho mbaya, wivu, visasi, unafiki.
Taifa hili lina mambo ya kustaajabisha kabisa, wapo watu wanafurahi watanzania wenzao waishi kama mashetaninashukuru sana mkuu nimeelewa sana.
hii husda naishuhudia sana kwenye jamii yetu.
mfano kuna mama mmoja kafanikiwa kitu ambacho ndugu na jamaa hawakutegemea, leo wote wamemnunia, hawampigii simu, wamekoswa raha kabisa ...
Haya ni mambo ambayo kama taifa lazima tuyatafakari upya, ni aibu sana katika karne hii mambo kama haya kutokea katika nchi yetuNi kweli kabisa.
Hatuwezi kuwa na Taifa la watu waadilifu kwa kubaguana.
Rushwa ni rushwa tu hata kama imefanywa na rafiki yako.
Utaogopwa na kuheshimiwa endapo hutamuonea aibu ndugu yako,rafiki yako, mwanachama wa chama chako,mtu wa dini yako na mtu wa kabila lako pale anapokiuka maadili na kwenda kinyume cha taratibu au pale anapotuhumiwa kutenda kosa.
Mfano Kama sheria inasema kuwa Msimamizi wa uchaguzi atamtangaza kuwa mshindi wa uchaguzi mgombea aliyeshinda kwa kura nyingi halafu yeye kwa kupewa rushwa ya madaraka au fedha akabadili matokeo na kumtangaza aliyeshindwa, basi hii ni moja ya dhulma na kujenga jamii iliyojaa dhulma kuanzia ngaza juu mpaka chini.
Kiongozi anayechaguliwa kwa wizi wa kura au kwa mabavu na kukiuka taratibu za wazi na za haki za kupiga na kuhesabu kura ni wazi kuwa huyo ni mtu aliyejawa na roho ya dhulma na ubaguzi.
Tukitaka tuwe na ujasiri na taifa la watu waadilifu ni lazima tuanze na mambo rahisi kabisa kama namna ya kupata viongozi kwa njia halali na kura halali.
Kama unashindwa kumwambia mwanachama mwenzako kuwa pole sana ndugu yangu uchaguzi huu umeshinda.
Na aliyekushinda naye ni mtanzania kama wewe hivyo hatuna sababu ya kumnyang'anya mtanzania huyo ili umpe mwingine na kuacha chuki na uhasama.
Huu ndio ustarabu na uadilifu.
Kwa sasa sijaona mtu wa namna hiyo hivyo ni lazima tuweke katiba mpya itakayowalazimisha waliopewa majukumu kuwa waadilifu.
Tuliitegemea sana serikali ya awamu ya tano kuwa itakua serikali ya watu waadilufu wasiojali vyama ,ukabila ,dini n.k lakini bado kuna kubeba chama kuliko kujenga utaifa.
Siasa zimezidi tena kwa kufanywa kwa mikono ya serikali.
TBC inashindwa kutuonyesha live Shughuli za Bunge lakini kutwa nzima inatuonyesha shughuli za uchaguzi wa chama cha mapinduzi.
Hatuonyeshwa jinsi sheria kandamizi na zile zinazoyagusa maisha yetu zinavyojadiliwa lakini tunaonyeshwa mambo ya siasa ya chama kimoja tu ambazo hazina umuhimu zaidi ya kampeni zisizoisha . Wakati huo huo tunaambiwa siasa mpaka 2020.
Nchi moja iliyopata uhuru miaka 57 iliyopita lakini ina watu wanaobaguana kuliko hata makaburu walivyokuwa wanawabagua waafrika kule S.A.
Haya ni mambo ambayo kama taifa lazima tuyatafakari upya, ni aibu sana katika karne hii mambo kama haya kutokea katika nchi yetu
rudia kidogo!Habari za asubuhi wana JF
Kwa masikitiko kabisa naomba niwasilishe hii hoja chungu. Taifa letu limejaa watu wanafki na wenye husda. Ni jambo la kawaida kabisa kuona watu wakimshangilia kiongozi au mtu mwenye pesa ambaye anafanya mambo ambayo siyo sahihi. Sehemu kubwa ya watu wetu ni watu waoga wenye tabia za kujipendekeza. Jamii yetu imejaa watu ambao furaha yao inakamilika pale ambapo mtu mwingine anaharibikiwa. Ikiwa mtu amefukuzwa kazi, au amefilisika, au amepatwa na matatizo basi jamii yetu inapata furaha.
Haya mambo ni ya hovyo kabisa kwenye jamii yoyote ile na kamwe taifa haliwezi kuendelea likiwa limesheheni watu wenye husda na unafki. Kwa mamtiki hiyo, itatuchukua miaka mingi sana kupata maendeleo tukiwa tunaendekeza wanafki na watu wenye husda. Watu wa aina hii wanarudisha maendeleo yetu nyuma. Kuna baadhi ya nchi kwenye bara la ulaya haswa karne zilizopita waliamua kuwaua wanafki, wachamwi (watu wenye husda) na washirikina wote. Hivyo basi, ni lazima tuwatambue wanafki na watu wenye husda kama ni maadau wa taifa letu na ndiyo watu wanaoturudisha nyuma kimaendeleo. NAOMBA KUWASILISHA, mapovu yanaruhusiwa.