Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,798
- 71,218
Katika taifa tunaloambiwa lina ukabila wa kiwango cha huu na ushindani wao wa kisiasa ulisababisha mamia ya watu kuuana, Basi inapofika mahali viongozi wanajishusha na kuombana radhi hadharani kama ilivyokuwa kwa Kenyatta na Odinga Basi hata maendeleo lazima yawepo kwani kuna muafaka wa kitaifa.
Sisi tunaponzwa na unafiki na chuki za sirisiri, usoni twajifanya tuna amani na upendo moyoni tunachukiana na kutafutiana mabaya mfano kesi na vifo. Tutakaa lini na kushirikiana kuleta furaha?
Ni bahati kuwa Watanzania wanaasili ya upole tuu, vinginevyo hali ya kisiasa ya sasa ingekuwa kwingine tayari matukio ya mauaji yangetamalaki. Katika ubinadamu hakuna mbabe kuliko wote, ndio maana watu kama Hitler alisalimu amri na kujiua. Gaddafi ameuawa kwa kudhalilishwa sana huku akilia machozi, Saddam aliveshwa kitanzi anyongwe akiwa na sura ya hudhuni sana kama vile hakupata kuwa mbabe kabisa.
Kabudi amewaambia Wakenya waache ukabila watuige. Je, na sisi hatuwezi kuacha chuki na KUWAIGA?