Qanyengere
Member
- Oct 22, 2014
- 60
- 1
Ni hospitali ya Muhimbili. Ewe Muhimbili ni kwanini unawaua waliokimbilia kwako wakiwa na full matarajio ya huduma bora na ya haraka licha ya ukubwa na umaarufufu wako? Ewe Muhimbili ni kwanini unaendelea kupokea wagonjwa mahututi ilhali huwashughulikii? Ewe Muhimbili ni kwanini basi usiwashauri wagonjwa kujitafutia sehemu nyingine ya miili yao kupatiwa huduma badala ya kuwasubirisha mauti? Bethlehemu kanza rafiki yangu alipatwa na ajali kiasi cha kuvunjika mguu wake, hiyo ni tarehe 02 - 10-2015 mkamtunza MOI wodi namba 18 sakafuni bila ya paracetamol wala kitu gani zaidi ya kuletewa chakula kutoka nyumbani kwao. Leo ni takriban wiki ya tatu mgonjwa hana hata tumaini la kushughulikiwa, je, huku ndiyo kutibiwa kweli? Kutoka hatoki, kutibiwa hakuna, je, la kufanya hamsemi sasa atasaidikaje? Ole wetu masikini tusioweza kwenda zetu apollo india tutaishia kuingia Muhimbili tusikopata matibabu. Pole kaka bethlehemu kanza najua si mapenzi yako lakini hii ndiyo Muhimbili yetu.