Tahadhari

Jidu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
1,232
Reaction score
757
Kumekuwa na wimbi la uhalifu kwa kutumia simu hivi karibuni.leo hii nilipokea simu kwa mtu asiyejulikana na kuniambia kuna Bonus ya tsh 10,000 anataka kunitumia kwenye a/c yangu ya NMB, nakunitajia yupo kwenye tawi fulani la NMB,hivyo nifanye hima kwa kumpa namba ya a/c yangu.

Akiendelea kuniaminisha kuwa ni mfanyakazi wa NMB na kuniambia hivi karibuni nilileta Fomu yangu ya uhakiki juu ya a/c yangu.Nilijua ni tapeli kwa kuwa kwenye zile fomu tunajaza a/c namba zetu iweje yeye ashindwe kujua a/c yangu?.nikaja gundua kuwa details zangu amaezitoa kwenye kampuni ya simu ambayo nimesajili namba yangu hivyo basi na waasa kuwa haya makampuni ya simu hayana siri juu ya wateja wake kwani imekuwa rahisi kwa hawa matepeli kujua jina la mtu na namba ya simu kiurahisi.

Hivyo chukueni tahadhari nimenusurika leo kesho inaweza mliza mwingine usikubali kutoa namba yako ya a/c ama ya siri kwenye simu hata kama atakuambia yeye ni GAVANA wa bank!Namba iliyonipigia ni hii 0784469847
 

Pole sana Mkuu. Hawa ni wezi wanatumia njia mbalimbali. Na kwa hakika hiyo simu itakuwa ni ya mtu mwingine. Kwa mfano kuna namna ambavyo wanaijua namba yako ya simu kutumia hata marafiki zako (ni mtandao mpana) then wana-disable namba yako na kuchonga kitambulisho chenye picha tofauti but jina ni la kwako wewe. Basi anaenda kibanda cha namba za simu anasema nimepoteza simu na line hivyo nataka kurudisha line yangu, akilulizwa kitambulisho anatoa na jina ni lako ila picha fake. Basi simu ikishakuwa hewani wanaitumia kwa uhalifu mwingi sana ikiwemo hata kupigia marafiki zako simu na kuwaambia watume hela au napifa toka kampuni ya simu fulani hivyo umeshinda mil kadhaa ili kupata labda tuma pesa au pia nipe namba ya a/c benki na ukiwapa cha moto umekipata. Ukiona simu card yako inakupa error au neno not recognised wahi haraka sana mtandao wa simu kurudisha namba vinginevyo utalia.

Wengine wanaiba hadi simu za mawaziri unasikia mimi waziri naongea hasa na wakuu wa taasisi akiwaambia eti nipe hela mtoto amefukuzwa ada na nitarudisha au pia kupiga kwa marafiki. Ni wengi wamelizwa na wanaripoti polisi but nashangaa hawa polisi hawatangazii umma ila wanabaaki kutangazia yale ya uongo tu. KOVA upo?
 
Bora ulivyo iweka namba yake humu.
Mkuu Mwita, hiyo namba tena unakuta ni ya mtu innocent kabisa ila wanakuwa wamei-hack. Soma post yangu hapo juu. Usishangae wewe siku moja unakuja kukamatwa na polisi kuwa umeiba kumbe ni majamaa wametumia namba yako kuiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…