iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Kumekuwa kukiripotiwa mauaji katika mkoa wa pwani na wilaya zake,na kimsingi yanalenga viongozi wa serikali
Wauaji hawa wanatumia silaha za moto,na kimsingi hawaibi chochote cha maana zaidi ya kuua na kuondoka.Mauaji ya aina hii si kwa nia ya kujikimu kiuchumi(kupata Mali)bali ni yenye mlengo wa watu fulani wenye itikadi fulani, na wanahisi serikali ndio tatizo lao.
Mauaji ya aina hii hufanywa zaidi na magaidi,magaidi hulenga viongozi wa serikali au taasisi za umma.
Mkoani pwani walengwa mpaka sasa ni Wenyeviti wa Vijijini,Vitongoji,na nadhani pia wajumbe
Hivi karibuni mkuu wa upelelezi wa wilaya aliuwawa,lakini waliomuua kimsingi hawakuwa na ajenda yoyote ya kiuchumi.
Nadhani kuna kundi/watu wenye mlengo hasi na jamii yetu na serikali kwa ujumla
Nashauri vikosi vya usalama vipige kambi mkoa wa pwani hata mwaka mzima,wapitie kila jambo na suala na kulitafiti kwa kina mpaka watu hawa wajulikane kabla hawajaleta madhara makubwa kwa taifa hapo baadae,
Kamati za ulinzi na usalama za vijiji na kata zinafanya kazi? Wakuu wa wilaya wana mikakati gani kuanzisha doria za usiku?
Sasa wanaua wenyeviti wa vijijini/mitaa,wakishakomaa watakuwa wanamlenga nani? Hata Boko Haram na makundi mengine yalianza hivihivi
Waziri wetu Mwigulu Nchemba aliwahi kuahidi kuunda kanda maalum,basi asichelewe,wakati akisubiri kuiunda,awe na kikosi kazi cha kufuatilia nyao za magaidi hao