Tahadhari: Wizi wa pesa kwa njia ya mtandao wa simu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
PHONE HACKING.jpg
CYBERCRIMINAL HACK YOU PHONE.jpg

WIZI MPYA

Kwa Watu wote wanaoutumia simu za mkononi, hii ni kwa ajili yenu na naomba uwe makini uisome hii na kuielewa.

Huu ni wizi mpya wa kutumia teknolojia ambao umeingia mjini kwa kitaalamu sisi wataalamu wa kuchokonoa simu tunauita “Swim Swap Fraud” na kuna baadhi ya watu tayari wamekwishalizwa.

Jinsi unavyofanya kazi

1. Mtandao kwenye simu yako unapotea ghafla, unaona imeandika “No Signal au Zero Bars” halafu baada ya muda unaona simu inaingia.

2. Hiyo namba iliyokupigia simu unakua huifahamu na inaweza kuwa ya mtandao wowote Tigo/Airtel/Halotel/TTCL/Vodacom na kadhalika kutegemea unatumia mtandao upi ambao muda huo sasa ndio unakuwa umekumbwa na hiyo shida ya kupotea potea kwa mtandao.

3. Huyo aliyepiga atakwambia kwamba kuna tatizo la mtandao kwenye simu yako na wewe utakubali kwa sababu kweli kuna tatizo. Atakuelekeza kubonyeza 1 ili tatizo la mtandao kwenye simu yako liweze kutatuliwa.
Akikupa maelekezo hayo usifanye lolote, kata simu.

Kwa sababu utakapobonyeza 1, mtandao wako utarudi ghafla na kisha kupotea (zero bars) na kwa kitendo hicho simu yako inakuwa imedukuliwa (hacked). Yaani kitaalam hao ndio ma-hacker

Wizi huu unaongezeka siku baada ya siku na kama una fedha kwenye akaunti yako ya simu (Tigo Pesa, Airtel Money, etc) basi zote zinatolewa.

Baada ya tukio hilo wewe utaona tu simu yako shida ni kwamba haina network lakini tayari wakati huo line yako ya simu inakuwa swapped na taarifa zote kwenye line yako anakuwa nazo huyo aliyefanya tukio.

Tatizo hapa ni kwamba hutapata taarifa zozote za kufanya kwa miamala ya aina yoyote kupitia simu yako kwa hiyo kwa wale wanaotumia USSD na Mobile Banking kuweni makini.

Wape faida na wengine
 
Shukrani kwa taarifa mkuu haijalishi taarifa tumewahi kuiona au hatujawahi, sharing is caring....... Ila Binafsi Sijaona kabisa mtu wa kuniibia kazembe namna hiyo hahahaha yan pesa inavyopatikana kwa shida mtu aje achukue kirahisirahisi namna hiyo et bonyeza 1 hahahahaha
 
View attachment 1177002 View attachment 1177005

WIZI MPYA

Kwa Watu wote wanaoutumia simu za mkononi, hii ni kwa ajili yenu na naomba uwe makini uisome hii na kuielewa.

Huu ni wizi mpya wa kutumia teknolojia ambao umeingia mjini kwa kitaalamu sisi wataalamu wa kuchokonoa simu tunauita “Swim Swap Fraud” na kuna baadhi ya watu tayari wamekwishalizwa.

Jinsi unavyofanya kazi
1
Mtandao kwenye simu yako unapotea ghafla, unaona imeandika “No Signal au Zero Bars” halafu baada ya muda unaona simu inaingia.
2
Hiyo namba iliyokupigia simu unakua huifahamu na inaweza kuwa ya mtandao wowote Tigo/Airtel/Halotel/TTCL/Vodacom na kadhalika kutegemea unatumia mtandao upi ambao muda huo sasa ndio unakuwa umekumbwa na hiyo shida ya kupotea potea kwa mtandao.
3
Huyo aliyepiga atakwambia kwamba kuna tatizo la mtandao kwenye simu yako na wewe utakubali kwa sababu kweli kuna tatizo. Atakuelekeza kubonyeza 1 ili tatizo la mtandao kwenye simu yako liweze kutatuliwa.
Akikupa maelekezo hayo usifanye lolote, kata simu.
Kwa sababu utakapobonyeza 1, mtandao wako utarudi ghafla na kisha kupotea (zero bars) na kwa kitendo hicho simu yako inakuwa imedukuliwa (hacked). Yaani kitaalam hao ndio ma-hacker
Wizi huu unaongezeka siku baada ya siku na kama una fedha kwenye akaunti yako ya simu (Tigo Pesa, Airtel Money, etc) basi zote zinatolewa.
Baada ya tukio hilo wewe utaona tu simu yako shida ni kwamba haina network lakini tayari wakati huo line yako ya simu inakuwa swapped na taarifa zote kwenye line yako anakuwa nazo huyo aliyefanya tukio. Tatizo hapa ni kwamba hutapata taarifa zozote za kufanya kwa miamala ya aina yoyote kupitia simu yako kwa hiyo kwa wale wanaotumia USSD na Mobile Banking kuweni makini.
Wape faida na wengine
Usiwatie hofu watu, hakuna upuuzi kama huu.
 
Back
Top Bottom