Tahadhari kwa Zitto Kabwe

Kwanza namsihi Zitto asisimamie pesa,asimamie umma wa Tanzania katika kumiliki uchumi wa nchi na haki za raia. Huu ni mtaji tosha kuliko pesa. Kina Nyerere walichangiwa pesa sembuse wewe? Kazana kaka hilo BARAZA LA VICHAA (BAVICHA) lina assigment maalum humu jf. Pengine sasa tutapata chama cha kizalendo cha ukweli
 

This is what a great thinker has to do. Big up mdau. Na bora angekuwa na histora njema ambayo haijaficha chembe yoyote ya UAMINIFU na Ukweli. Hapa atafikia kipindi kile cha Mrema ambay sasa ndiyo amepotea kabisa na hana hata kauli. kila wakati Heshima, Utii, mapatano na kuthamini utu wa kila mtu utakupelekea kustawi. Hapa ndionmwanzo mgumu wa Zitto graf yake kwenda chini. Na zaidi ni kuwa migogoro mikubwa itakikumba chama chake pia kama taasisi ilivyokuwa Chadema. Atagombea uenyekiti miaka mingapi?? ajua mwenyewe na huo uraisi anaoutamani ni ndoto za mchana kabisa. Angalibaki chadema na akatii angefikia ndoto hiyo ila ACT ni shimbo ya Gehena.
 
Hivi maelengo ya ACT kama chama cha upinzani ni yepi? Ni kwa namna gani kitakuwa tishio kwa CHADEMA? Naomba kufahamishwa.

Hilo ndilo linalotupa shaka watazamaji hivi hiyo ACT (T) lengo lake ni kushika dola? Au kupambana na CDM?
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Kumbe siyo chama cha upinzani!kipo kushindana na chadema!sasa ndugu yangu kama ndiyo matarajio yako hayo,utakufa kwa presha,ngoja uone jinsi cdm inavyochukuwa dola!
 


Tatizo lako unaandika mambo ya kufikirika tu hujui ugumu wa safari ya Zitto. Mbali na huo Usaliti wake ni shida sana. Hana wa Kumsafisha popote zaidi ya kupoteza tu. Anategemea pesa za CCM zitafika mahali pesa hizo zitaisha kwani CCM hawana nia njema kusaidia kuanzisha ACT. Kila uchaguzi kikaribia chama kipya kinaanzishwa kwa msaada wa CCM kikiamini kupunguza upinzani wa vyama makini. Msishangilie sasa kwa kuwa ACT ni kama CCJ. Hatuamini maneno matamu bali utendaji na uaminifu. Zito anatamani kila kitu na atakosa vyote kwa kuwa ni Msaliti.
 
Zitto atakuja sana kumlaumu Kitila Mkumbo. Mambo yakianza kukwama tu Zitto ataanza kumtafuta mchawi wake. Na hapa ndipo Kitila Mkumbo atakapoanza kutofautiana na Zitto.

Kwahiyo unafikiri angefanya nini ,hebu jaribu kutuonesha mbadala.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Mkuu aim ya ACT ni ipi haswaaa? Kupambana na Chadema au kushika dola?
 
Zitto alijiona yupo juu ya chama aende kujenga chama chao cha wasaliti ACT. Yeye anadhani kujenga chama cha siasa ni kazi rahisi aende kuijenga ACT tuone sasa
 
ACT sawa....sawa ....kabisa.Vizuri nawe ukajiunga na UKAWA kutupunguzia mzigo sisi wenye elimu ndogo ya siasa....Umoja ni Nguvu na Uhuru ni Kazi.
Naunga mkono hoja. Ni bora act ijiunge ukawa lakini act kuitusi cdm ni utoto wakisiasa.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiki chama kitakuja kuwa tishio kwa Chadema, wait and see...ZZK ana wafadhili wengi ndani na nje ya nchi...wewe waache tu hawa kina Mtei na Mbowe waendeleze ukabila, udini na ukanda ktk hiyo NGO yao!...

Tishio kwa CHADEMA tena ?
Ina maana hiki kigenge kimeanzishwa Mahsusi kutishia CHADEMA?
 

Katika maisha ni kuchukua risk, ili mradi tuu ziwe calculated risk. Zitto anaweza kushinda anako kwenda lakini nimpe sifa za kugoma kujiunga CCM na kwasababu hakuna chama ambacho kinasimamia misingi ya haki na usawa basi kilichobaki ilikuwa ni kujiunga na ACT.

Zitto amakuwa sana kisiasa, wote tunajua kujenga chama sio kazi raisi, lakini sidhani kama Zitto na Kitila wanatengeneza platform ya national politics ndani ya 5 years, nadhani wanatengeneza platform ya regional politics kwanza. Maana kwamba Zitto hatoshindana Kigoma Kaskazini sababu hilo jimbo ni safe harbor yake, atakachofanya yeye ni kugombea Kigoma mjini ambapo most likely atashinda Landslide. Kigoma Zitto anaweza kuwipe majimbo yote au akashindwa moja. Anachoitaji ni wabunge 5-10 kwenye uchaguzi huu. Kwa nguvu hii ya Ukawa na ugawaji majimbo strong candidates wa UKAWA watakao katwa basi ni wazi kabisa wanakwenda ACT hakuna mjadala.

Sasa kama unajua siasa na ufahamu analysis hii ni njapanda kubwa sana kwa wapenda upinzani, maana wanagawiwa sawa kwa sawa matokeo yake CCM anatambaa kama kawaida. Hii risk inaweza kuwa mwisho wa Zitto au mwanzo wa siasa mpya kabisa nchini Tanzania.
 

I like your way of reasoning!
 
Kila nikisoma maandishi ya washabiki wa Zitto (na ACT?) inaonyesha matumaini ya chama chao yako kwa mtu (Zitto) na Maumivu ya chadema ambayo yanaaminishwa na mashabiki wa ccm. Survival ya chama hiki itakuwa wakishinda angalau idadi kadhaa ya wabunge, na inavyoonekana wanatumaini kusaidiwa na chama tawala kama njia ya kuwadhibiti wapinzani wao ndani ya bunge. Hii isipotokea tutashuhudia mwisho wa ACT. Na ikiwa bahati mbaya Zitto akashindwa kurejea bungeni na hata kama chama chake kitakuwa na wabunge hilo nalo litakuwa tatizo jingine labda akibadilika kitabia na kimatendo.
 
I Kigoma Kaskazini unaposema ni safe harbour kwa Zitto si sahihi Ukiangalia matokeo yake ya kwanza na ya uchaguzi uliopita. Anakukimbia huko kwa sababu anajua yaweza kuwa ngumu kwake kushinda. Siasa za kigoma tunajua ni za upinzani, lakini huwezi kuwatoa kabisa chama tawala. It is a risk undertaking, ikiwa bahati mbaya akashindwa kupata ubunge na wabunge sijui kama anayo subira ya miaka mitano. Lakini pia yawezekana kwake haikuwa rahisi kwenda ccm kwa sababu maalumu ikiwemo pia uwezekano kwamba huko hasingetimiza matarajio yake?
 
Changamoto kubwa ipo mbele yake!! kama ataendelea kusikiliza maneno ya wapambe wake na siasa za kuihujumu CDM mwisho wake utakiwa mbaya zaidi.

Hivi Zitto anaujasiri gani kwa sasa wa kuichachafya CCM? wanamfaham A to Z. Mnafikiri wale akina Kibajaji na Ngeleja ni wajinga sana kiasi hicho kwa kuropoka maneno yale? Ni kwa sababu bado mfumo unamuhitaji ndio maana wanapotezea wasimuabishe!!

The moment atakapoonekana the really threat kwa CCM ndiyo wakati muafaka watakapomuacha uchi. Ila kwa sasa kwakua anapambana na adui wao mkuu ni kipenzi kupitiliza!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…