Tahadhari kwa wanaotembelea Hifadhi za Saadani

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Hifadhi hii iko chini ya TANAPA, ilianzishwa mwaka 1962 ikiwa ni pori la akiba. Mwaka 2005, ilipandishwa hadhi rasmi na kuwa hifadhi ya taifa.

Mbuga hii ipo Mikoa ya Pwani na Tanga, kwa upande wa Kaskazini ipo Wilayani Pangani, Bagamoyo (Kaskazini) na Zanzibar.

Dar es Salaam. Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka wakazi wa Dar es Salaam wanaotarajia kutembelea Hifadhi za Taifa za Saadani kutotumia njia ya Mkurunge Bagamoyo kwa kuwa miundombinu yake imeharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Meneja wa Mawasiliano wa TANAPA, Paschal Shelutete imeeleza kuwa miundombinu, ikiwamo madaraja na barabara vimeharibiwa na mvua.

“Hivyo basi wananchi na watanzania wanaotarajia kutembelea Hifadhi za Saadani wanashauriwa kupitia njia ya Msata-Mandera hadi Saadani na kwa wageni wanaotokea Tanga wanashauriwa kupitia njia ya Pangani-Mkwaja hadi Saadani,” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
nimekuja fasta nikajua popobawa karudi,asante kwa taarifa anyway!
 
Asante maana nilianda tour jumapili hii kwenda saadani.
b5cc98a0577f442cda7c2b6b79e258ed.jpg
 
kwa mvua hizi wanaoenda wanaweza kushindwa kuingia mbugani kwa sbb ya barabara kuharibika na udongo kiasi kikubwa mfinyanzi
 
Dah, tangazo limefika wakati mwafaka, maana nilitaka kuelekea huko weekend hii kutokana na lile tangazo la Makamba.
 
Back
Top Bottom