Tahadhari kwa mnaobeti: Azimia baada ya mkeka wake kuchanika

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,476
4,448
Jana usiku ulikuwa mchungu kwa jamaa mmoja aliyekuwa katika chumba cha kuchezeshea kamari "Betting"eneo la Magomeni kagera.

Akiwa anafuatilia mpambano kati ya Sevilla vs Real Madrid aliweka rehani pikipiki yake na pesa taslim 400,000 kuwadhamini Real Madrid kwamba watapata goli kuanzia 85+,kilichotokea ni mshambuliaji wa Sevilla aliyejiunga wiki iliyopita kutoka inter Milan kushindilia msumari kwa mzungusho hatari au unaweza kuita ndizi na kumuacha kipa wa Madrid Keylor Navas asiwe na cha kufanya na kuzima ndoto ya jamaa huyo

Jamaa huyo kwa mshangao na pressure alitoa sauti moja ya mshangao na kisha kuanguka chini " kuzimia" ..watu walimpa first aid kwa kumpepea nk nk

1.Wacheza betting acheni kukariri unamuua Sevilla Sanchez Pizjuan tena muda ambao yeye ndio anashambulia

2.Kaa mbali na betting kama wewe huwezi kuhimili pressure

Mwisho betting haifai ,faida kiduchu na hasara kubwa
 
Duuuh iko poa ila kubet ni kitu iliyoko damuni mtu kuacha hadi Aende Soba house chini ya ulinzi mkali zaidi ya Chid na ray c. ...
 
kila siku nakula biere naweka gari full tank kwa pesa za betting.siwezi kuacha kubeti sababu nasomesha watoto pia kwa kubeti kila wiki nampasua Kanjibai we leta mijungu yako ila haisaidii
 
Mkuu c uwe unantupia odds tumbutue wote
 
Kubeti ni kamari, na kamari ni haram....siku pumzi ikiisha ndio utajuwa kuwa kamari ni haram.....
Hakuna kitu kama hicho, kubet sio haramu wala sio dhambi labda kwa dini nyingine lakini kwa mimi mkristo tena msomaji mzuri wa biblia sijawahi kukutana na andiko lolote linalosema kubet ni dhambi kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana. Na siku zote tunaishi kwa kufuata nw kuheshimu neno la Mungu ambalo limeandikwa kwenye vitabu vitakatifu. Mungu alimpa Musa amri kumi tu kwamba ukizitii hizo basi utakuwa umefanya mapenzi ya Mungu. Hayo mengine mnayokatizia kama ya kubet mnajitungia tu na kupotosha watu, tena ninyi ndiyo mtakuwa wa kwanza kuonja adhabu ya mauti
 
Hapa ninayo mikeka yangu minne nasubiri ila mm ndiyo nimekuwa mgonjwa kabixa nisipo weka mkeka sina usingizi kabixa nitateseka sana ila nikiweka raha sana
 
Jana usiku ulikuwa mchungu kwa jamaa mmoja aliyekuwa katika chumba cha kuchezeshea kamari "Betting"eneo la Magomeni kagera.

Akiwa anafuatilia mpambano kati ya Sevilla vs Real Madrid aliweka rehani pikipiki yake na pesa taslim 400,000 kuwadhamini Real Madrid kwamba watapata goli kuanzia 85+,kilichotokea ni mshambuliaji wa Sevilla aliyejiunga wiki iliyopita kutoka inter Milan kushindilia msumari kwa mzungusho hatari au unaweza kuita ndizi na kumuacha kipa wa Madrid Keylor Navas asiwe na cha kufanya na kuzima ndoto ya jamaa huyo

Jamaa huyo kwa mshangao na pressure alitoa sauti moja ya mshangao na kisha kuanguka chini " kuzimia" ..watu walimpa first aid kwa kumpepea nk nk

1.Wacheza betting acheni kukariri unamuua Sevilla Sanchez Pizjuan tena muda ambao yeye ndio anashambulia

2.Kaa mbali na betting kama wewe huwezi kuhimili pressure

Mwisho betting haifai ,faida kiduchu na hasara kubwa

habari yako ya uongo uongo tu, hiyo kampuni gan wanayoweka pkpk
 
Back
Top Bottom