Tahadhari kwa dr slaa na mbowe

Tahadhari kwa dr slaa na mbowe

Joblube

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2011
Posts
369
Reaction score
151
Napenda kuwapa tahadhari Dr Slaa na Mbowe vurugu zote zinazoendela hapa mtandaoni walengwa wa kuu ni nyie. Mzee wa Pembe za ndovu anapambana kufa na kupona baada ya kugundua kuwa chama chake kipo kwenye hali mbaya kabisa hasa baada ya kutambua kuwa hakiwezi kupambana tena na CHADEMA kwa hoja. Huyo jammaa ametengeneza kukundi kidogo cha kupambana na CHADEMA mitandaoni kwa kujisajili kwa ID mbalimbali. Kikundi hicho kimepewa kazi ya kushinda JF kujenga hoja za kuichafua CHADEMA. Lengo kuu la huyu strategist wa magamba ni kuhakikisha mmoja wenu anaingia kwenye malumbano na Mtu wao waliomtengeneza ili kuipunguza nguvu CHADEMA, kwa hiyo mkakati wao ni wa long term kupambana mpaka 2014 kuhakikisha mnaoingia kwenye mgogoro wa kurushiana maneno na huyo mtu wao. Naomba mjiulize mtu huyu alishasema hatagombea uongozi wowote ndani ya chama hata nje ya chama lakini wao wanampamba kuwa anachukiwa kwa kuwa anautaka U/nyekiti, upi huo na alishasema hagombei.Kuelekea 2014 jiandaeni kisawasawa mtapitishwa kwenye tanuru la moto kuliko hivi sasa. Jipeni moyo kwa kuwa mkipita hapo ukombozi ndio utakuwa umekaribia. Pale Makoa Makuu msimwamini yeyote mbinu zinazotumiwa ni za hali ya juu katika kuwanunua viongozi wenu kuweni na utaratibu wa kutilia shaka kila dalili zinapojitokeza ni wakati wa kukesha bila hivyo mtakatwa ki-dizaini mzee wa pembe za ndovu si mchezo.
 
Mmmmmmmmmh cheap arguments .....!!!! mr CIA aka secret agent!!!
 
we dogo naona unataka kung'olewa kucha na meno au kuchomwa sindano ya sumu. ohooo..Shauri yako.
 
Though it's a sell-by-date product you will surely get buyers!Good luck!!!
 
Yote haya kayataka mtoto wa baba wa taifa yericko julius nyerere. Hawa maccm yametumia porojo za last born wa butiama kutuattack.
Tunawalaumu maccm wakati walioasisi ni hawa vifaranga na mama zao.
 
Hizo fedha za rushwa za magamba wana CDM chukueni tu, kuleni na nyingine changieni CDM na kisha msifanye lolote!!
 
Kuna ukweli, post nyingi humu ni za ccm na lengo ni kuonyesha kuwa kuna mgogoro CHADEMA. Ni heri kukaa kimya na kuwafuatilia wenye nia ya kukosanisha na kisha kuchukua hatua makini ambazo zitawaacha wameduwaa. Naiamini CDM, kwa sababu siku zote imekuwa makini na huchukua hatua zote kwa umakini na werevu wa hali ya juu.
 
Werevu tulishaliona hilo kitambo. Ila ni jambo zuri kutia msisitizo
 
wewe ni mmoja wa wale usalama wa CDM (UWC) walioandika ule waraka?
 
Napenda kuwapa tahadhari Dr Slaa na Mbowe vurugu zote zinazoendela hapa mtandaoni walengwa wa kuu ni nyie. Mzee wa Pembe za ndovu anapambana kufa na kupona baada ya kugundua kuwa chama chake kipo kwenye hali mbaya kabisa hasa baada ya kutambua kuwa hakiwezi kupambana tena na CHADEMA kwa hoja. Huyo jammaa ametengeneza kukundi kidogo cha kupambana na CHADEMA mitandaoni kwa kujisajili kwa ID mbalimbali. Kikundi hicho kimepewa kazi ya kushinda JF kujenga hoja za kuichafua CHADEMA. Lengo kuu la huyu strategist wa magamba ni kuhakikisha mmoja wenu anaingia kwenye malumbano na Mtu wao waliomtengeneza ili kuipunguza nguvu CHADEMA, kwa hiyo mkakati wao ni wa long term kupambana mpaka 2014 kuhakikisha mnaoingia kwenye mgogoro wa kurushiana maneno na huyo mtu wao. Naomba mjiulize mtu huyu alishasema hatagombea uongozi wowote ndani ya chama hata nje ya chama lakini wao wanampamba kuwa anachukiwa kwa kuwa anautaka U/nyekiti, upi huo na alishasema hagombei.Kuelekea 2014 jiandaeni kisawasawa mtapitishwa kwenye tanuru la moto kuliko hivi sasa. Jipeni moyo kwa kuwa mkipita hapo ukombozi ndio utakuwa umekaribia. Pale Makoa Makuu msimwamini yeyote mbinu zinazotumiwa ni za hali ya juu katika kuwanunua viongozi wenu kuweni na utaratibu wa kutilia shaka kila dalili zinapojitokeza ni wakati wa kukesha bila hivyo mtakatwa ki-dizaini mzee wa pembe za ndovu si mchezo.

uongee na yule mtembea na sumu sababu nyie chanaga united na mungu wenu wa Tengeru mnajua mlifanyalo
 
Lamsingi kitengo cha ulinzi kiimalishe ulinzi na intelegensia ya CDM iwe makini kwa kufatilia kila tukio.
 
Back
Top Bottom