Tahadhari juu ya Lowassa

ulimbo lunopo

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
243
Reaction score
39
watanzania wenzangu tumekuwa tukimwona waziri huyu aliyetolewa kama chambo kujiuzuri ili kuwaficha wengine kwa kashfa za kuiba rasilimal za walalalahoi wa TANZANIA!!! Mtu huyu anapita makanisani na misikitini kufanya harambee ikiwa kama sehemu ya kujisafisha! Hivi sasa ameingia hadi kwa wasanii' NYENZO YAKE KUBWA NI PESA, ana jeuri ya pesa ANAGAWA PESA KAMA NJUGU.!! Hiv wananchi wenzangu hebu tujiulize maswali machache tu kama tahadhari..

Hizo pesa huyu bwana mkubwa anazitoa wapi?? Mbona vyanzo vyake vya mapato alivyoweka hadharani haviendani na mabilion anayoyamwaga kila uchao??

Kuna wakati alisema hizo fedha anasaidiwa na rafiki zake!! Sasa ndugu zangu hamuoni kwamba wale watu wanaomsaidia watataka na yeye awatendendee fadhila akapoingia madarakani ??KUMBUKA,HAKUNA KITU CHA BURE DUNIANI,,,

JAMANI MTU HUYU TUMUANGALIE KWA MACHO MATATU! Ana njaa ya URAIS ILI AFANIKISHE MAMBO MAKUU MAWILI

1, KULIPA KISASI KWA WOTE AMBAO HAWAPO UPANDE WAKE! nadhani wanafahamika, mfano SITA

2, KURUDISHA MABILION ANAYO INVERST KWENYE HUO MCHAKATO WA URAIS.

tafakari! Chukua hatua!!
 
Hivi lini alisema anataka kuwa rais? Mbona mnaweweseka namna hii?
Na hata akitaka kugombea ni haki yake kikatiba kama mtanzania,suala nani anafaa nani hafai waachieni wananchi ndio wataamua,
Kama wewe unamuona hafai sawa lakini tupo wengi tu tunamuunga mkono subiri atangaze nia na kura tutampa
 
Lowassa ni janga kuu la taifa!!! Watanzania wanapaswa kulielewa hili na kuweka ushabiki pembeni...Makanisa na Misikiti wanaonyesha udhaifu mkubwa juu ya fedha chafu za Lowassa!!
 
Zingine ni fedha fake,makanisa inabidi yanunuwe cash counting and detecting machines.

Aliishawahi toa mipesa ifakara alafu baada kama wiki moja minote fake ikatakapaa mitaani.
 
Kama tatizo ni ufisadi uliopelekea kujiuzuru na kwamba Richmond ndio tatizo .....Why ibadilishwe jina na kisha iwe nzuri kwa mitambo ile ile na Obama azindue?? Tafakari na tambua siasa changa na chafu. Siasa za maji taka hizi.
 
Vijana hizo pesa mkiacha kuchukua mtakua hamuendani na kizazi hiki.Hizo ni hela zenu chukueni.

Kuwakomesha ni kuzichukua then unafanya maamuzi ya kizalendo.Pongezi kwa vijana wa bodaboda Arusha na wamachinga kanda ya ziwa
 
Naam ni kuzitafuna tu huu ndo wakati wenyewe!! Kie kie kie
 
Acha kuwasemea wengine.kama wewe ni fisadi sawa. unaweza wasemea mafisadi wenzeko
 
Mimi sina itikadi ya chama chochote ila 2015 akisimama Lowassa basi nampa kura yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…