Tahadhari: Barabara ya Tengeru ni hatari

Tahadhari: Barabara ya Tengeru ni hatari

Panthera 1

Member
Joined
Dec 30, 2014
Posts
50
Reaction score
9
Mnamo mwaka jana tulileta malalamiko na kuyaandika mtandaoni ili kilio chetu kisikike lakini hakuna yeyote aliesikia hilo wala kuchukua hatua.
Naamini wahusika wanafahamu hilo kwamba siku chache zilopita barabara ya kutoka soko la tengeru hadi kuingia geti la taasisi ya mifugo tengeru ilikuwa imechimbwa na greda na hivyo kuacha vumbi zito chini ambalo pindi magari ya pitapo au pikipiki basi usababisha vumbi zito kupeperushwa juu na kuwa kero kwa wapita njia kutokana na uchafu wanaoupata kutokana na vumbi hilo ambalo wahusika wanauwezo wa kumwaga maji ya kutosha na kuifanya barabara hiyo kuepuka vumbi hilo.
Licha ya uchafu unaotokana na vumbi hilo pia hali ya usalama wa kiafya utakuwa hatarini kutokana na kuvuta pumzi kutoka katika vumbi hilo.
Isitoshe,barabara hiyo imenyooka sana na kufanya toyo na magari kupita mwendo wa kasi sana na hakuna hata tuta moja katika barabara hiyo.
Ikumbukwe kwamba,barabara hiyo imepita katika hotel ya Serena na kuishia ktk geti la kuingilia Chuo cha Mifugo Tengeru.
Ni vyema kuchukua tahadhari mapema na wahusika kulishughulikia hilo mapema na haraka.
CHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARI.
 
Back
Top Bottom