simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,418
- 9,206
SIKU YA WAJINGA DUNIANI.
=====
Leo ni siku ya wajinga duniani maarufu kama April fool, ni siku ambayo kimazoea watu hufanya mzaha kwa watu wengine na endapo watahadaika na huo mzaha basi wataitwa wajinga na hii siku itakua yao.
Kwa baadhi ni siku itakayoleta usumbufu mkubwa inayoweza kuwapa maumivu ikiwemo ya moyo au fedha. Kuna watu watatoa taarifa zilizochupa mipaka kiasi kwamba mtu anaweza asikumbuke kama leo siku ya wajinga kutokana na ukubwa wa taarifa anazopewa.
Niwakumbushe wapewa taarifa kwamba leo ni siku ya wajinga hivyo kabla hawajakumbwa na taharuki waikumbuke siku ya leo katika mizani yao ya kufikiria pia niwakumbushe watoa taarifa, kama ni lazima wao washiriki siku hii basi wapime taarifa za kutoa na nani wa kumpa. Mtoe mzaha usioleta madhara ambao wewe na unayempa taarifa mtaishia kucheka kwa pamoja jinsi ulivyomtega akashindwa kutegua, taarifa kama misiba, kuna watu mioyo yao haiwezi kuhimili na anaweza kutupa simu kabla hujamalizia kusema siku ya wajinga na kuzua sintofahamu isiyohitajika.
Casuist