Tafsiri za Namba ki-Biblia;Kitendawili unachopaswa kukitegua.

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,500
2,056
Sabalkheri wanaJamii Forums!

Ni Jumapili tulivu kabisa iliyo na Neema kwetu binadamu, kama una siha njema ni Jambo la kumshukuru Mungu.Poleni na Ibada na pia poleni ndugu zangu wa Madhehebu ya Dini ya Mashariki ya mbali mnaoendelea na Mfungo.

Mungu awape Busara, Hekima, Unyenyekevu na kuyafanya yanayompendeza Allah hususan kwa kipindi hiki kigumu mnachopitia.Pia baada ya Mfungo muendelee na nidhamu hii hii mnayoionyesha kwa Allah kwa kipindi chote cha maisha yenu kwa kadiri mtakavyojaaliwa na siyo tu kwa kipindi hiki cha mpito.

Kwa kuyafanya hayo machache, basi unaitwa Muislam msafi kama neno islam linavyosadifu tafsiri takatifu ya Usafi mbele za Mungu.

Nirudi kwenye Mada.Si mara moja au zaidi umewahi kusikia kuwa namba zina tafsiri, Ipo tafsri ya kidunia na pia ipo tafsiri ya Kiimani/Kiroho (Biblia).

Tafsiri ya kidunia kuhusu namba siijui vizuri, Ninafahamu japo kwa ufupi tafsiri ya Namba Kibiblia kama ambavyo zimetumika mara kadhaa katika Maandiko.

Unaweza kuwa na ufahamu zaidi ya nitakayoyaweka humu, kama ndiyo basi naomba "Uongezee nyama palipopunguka" ili tuweze kujifunza sote kwa pamoja.Na Mungu atakubariki.

Maana ya Namba Moja (1)

Namba Moja humaanisha Umoja au Muungano katika Biblia.Kwa mfano, Yesu alimwomba Mungu kwamba wafuasi wake “wote wapate kuwa kitu kimoja, kama vile ambavyo wewe, Baba, umo katika muungano pamoja na mimi na mimi nimo katika muungano pamoja na wewe.Yohana 17:21; Mathayo 19:6.

Maana ya Namba Mbili (2)

Katika mambo ya kisheria, mashahidi wawili huthibitisha ukweli wa jambo fulani. (Kumbukumbu la Torati 17:6) Vivyo hivyo, kurudia maono au maneno fulani kulihakikisha kwamba jambo hilo lilikuwa hakika na la kweli. Kwa mfano, Yosefu alipokuwa akifasiri ndoto ya Farao wa Misri, alisema hivi: “Kwa kuwa ndoto hiyo ilirudiwa mara mbili kwa Farao inamaanisha kwamba jambo hilo limewekwa imara na Mungu wa kweli.” (Mwanzo 41:32) Katika unabii, “pembe mbili” zinaweza kuwakilisha serikali pacha, kama vile nabii Danieli alivyoambiwa kuhusu Milki ya Umedi na Uajemi.—Danieli 8:20, 21; Ufunuo 13:11.

Maana ya Namba (3)

Sawa na vile mashahidi watatu wanavyoweza kuhakikisha kabisa jambo fulani kuwa la kweli, kurudia jambo mara tatu kunakazia au kuonyesha kwamba linalosemwa ni hakika.—Ezekieli 21:27; Matendo 10:9-16; Ufunuo 4:8; 8:13.

Maana ya Namba (4)

Namba hii inaweza kumaanisha ukamili katika umbo au katika utendaji, kama vile katika maneno “pembe nne za dunia.”—Ufunuo 7:1; Isaya 11:12; Ufunuo 21:16.

Maana ya Namba (6)

Kwa kuwa namba hii imepungua saba inayowakilisha ukamilifu, sita inasimamia kutokamilika au lisilo kamilifu, au jambo linalohusianishwa na maadui wa Mungu.—1 Mambo ya Nyakati 20:6; Danieli 3:1; Ufunuo 13:18.

Maana ya Namba (7)

Mwanzo 2;1-3

1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.

2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Namba saba hutumiwa mara nyingi kumaanisha ukamilifu au Utakaso. Kwa mfano, Waisraeli waliagizwa na Mungu kuzunguka jiji la Yeriko kwa siku saba, na kuizunguka mara saba katika siku ya mwisho. (Yoshua 6:15) Biblia ina mifano mingi ambapo namba saba imetumiwa kwa njia hiyohiyo. (Mambo ya Walawi 4:6; 25:8; 26:18; Zaburi 119:164; Ufunuo 1:20; 13:1; 17:10) Yesu alipomwambia Petro kwamba amsamehe ndugu yake “si, Mpaka mara 7, bali, Mpaka mara 77,” kurudia namba 7 kulionyesha kwamba alipaswa kuendelea kusamehe “bila kuacha”.—Mathayo 18:21, 22.


Maana ya Namba (10)

Namba hii inaweza kuwakilisha jumla ya kitu, au kukusanya pamoja.—Kutoka 34:28; Luka 19:13; Ufunuo 2:10.

Maana ya Namba (12)

Namba hii inaweza kumaanisha ukamili kuhusiana na kusudi la Mungu. Kwa mfano, mtume Yohana alipewa maono ya kimbingu ambapo aliona jiji lililokuwa na “mawe ya msingi kumi na mawili, na juu ya hayo majina kumi na mawili ya mitume.” (Ufunuo 21:14; Mwanzo 49:28) Namba 12 ikizidishwa mara kadhaa pia inaweza kuwa na maana hiyohiyo.—Ufunuo 4:4; 7:4-8.

Maana ya Namba (40)

Baadhi ya hukumu au adhabu ilihusianishwa na namba 40.—Mwanzo 7:4; Ezekieli 29:11, 12.


Nawatakia Jumapili Njema.
 
Bible ni kitabu kilichobeba masomo mengi, ukiachana na spirituality ndani yake kuna masomo kama numerology(somo la namba), astrology(au huitwa astro-theology) mfano samaki wawili ambao yesu alilisha watu ni moja ya zodiac sign ambazo zipo 12,wale samaki wawili ni sign of picses.
Pia kwenye bible kuna mkusanyiko mkubwa wa secret doctrine kama esoteric writtings, kabala writtings, ambazo maana zake ni tofauti na tunavyotafsiri somo kwenye bible, mfano sabato tuijuayo waumini ni tofauti na sabato inayozungumziwa kwenye bible. Mfano adam tunaemjua kwenye bible ni tofaut na tulivyoelewa.
Jesus died at age of 33, yesu alianza kazi ya bwana akiwa na mri wa miaka 12,etc all these ni astrology.wenye wanaita astro-theology.
 
Back
Top Bottom