Tafsiri ya Lugha ya Picha Rais aliposema atakua Rais wa Wanyonge.

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,234
Wakuu Wanyonge ni watu gani Mimi sinapata maana halisi ajira zipo kwa watu waliokua na ajira zao basi kama ulikua huna ajira serikalini at least uwe mwanachama hai ndani ya CCM.

Matukio ya Njaa na majibu waliyopewa wananchi yananifanya niulize Wanyonge ni wapi? Wanyonge ni akina nani?

Waathirika wa tetemeko la Bukoba nao wanazidisha mimi kuhoji wanyonge ni kina nani?
 
Wanyonge kwake ni machinga, labda sababu ulikuwa ni mtaji wa wapinzani, mkulima ni mali ya CCM tayari hivyo hahitaji kumbembeleza, mhitimu wa chuo sio mnyonge hata kama hana ajira
 
Wanyonge kwake ni machinga, labda sababu ulikuwa ni mtaji wa wapinzani, mkulima ni mali ya CCM tayari hivyo hahitaji kumbembeleza, mhitimu wa chuo sio mnyonge hata kama hana ajira
Wamachinga kwa sasa wanapanga bidhaa zao kwa raha mstarehe hapo mjini kati, wakulima nao debe moja la mahindi kwa Ng'ombe 3.
 
Kwa kweli ni ngumu sana kuelewa dhamira ya kilanja, unapowachukia matajiri kwa kudhani unawasaidia masikini matokeo yake ndio haya tunayokumbana nayo, matajiri wamebaki na utajiri wao ile pesa waliokuwa wameiweka kwenye mzunguuko wameitoa hawana hakika ya kesho kilanja ataongea nini, tumebaki tunashangaa, kilanja alipotishia atabadili fedha wakanunua hela ya malkia na ya George Washington hali ni tete madeni hayalipiki baadhi tumepoteza nyumba ukipata leo unashukuru hujui kesho utakula nini, kifupi tumerudi miaka 20 nyuma, ya Mkapa na Kikwete yote yanapotea, kwamba hela ipotee mifukoni ni sifa kwa kilanja, lakini ukiangalia zimepotea kwa hao wanyonge wanaotetewa matajiri wamebaki na utajiri wao, tujiulize kati ya tajiri na mnyonge nani amepoteza, nani ameumia na nani anaelalamika?
 
Wakuu Wanyonge ni watu gani Mimi sinapata maana halisi ajira zipo kwa watu waliokua na ajira zao basi kama ulikua huna ajira serikalini at least uwe mwanachama hai ndani ya CCM.

Matukio ya Njaa na majibu waliyopewa wananchi yananifanya niulize Wanyonge ni wapi? Wanyonge ni akina nani?

Waathirika wa tetemeko la Bukoba nao wanazidisha mimi kuhoji wanyonge ni kina nani?
watu wa chato!
 
Back
Top Bottom