Tafsiri ya Baraza dogo la Mawaziri

Tafsiri ya Baraza dogo la Mawaziri

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Kuna wakati Mwalimu Nyerere alipata kuulizwa juu ya uwepo wa Wakatoliki wengi kwenye Baraza aliloliunda. Mwalimu alishangazwa na swali hilo, na alijibu, kuwa alichoangalia yeye wakati wa kuunda baraza ni mahitaji ya Watanzania, na hivyo, aliwatafuta wale wenye uwezo na sifa za kufanya kazi itakayokidhi mahitaji ya Wananchi walio wengi.

Tunaona mpaka anapolitangaza Baraza lake, Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli alikuwa bado hajawapata mawaziri wanne wenye uwezo na sifa za kujaza nafasi kwenye wizara nne.Ni dhahiri, si kila mmoja ataridhika na baraza hilo dogo la mawaziri. Pamoja na ukweli kuwa mamilioni ya Watanzania wameonyesha kulikubali baraza, bado, siku zote, zitajitokeza sauti za wenye kubeza .

Hata hivyo, ni ukweli kuwa , kwa Rais Magufuli kuchukua muda mrefu kufanya tafiti za kina juu ya mahitaji ya Watanzania, na kwa kuangalia uwezo na sifa za atakaowateua, imedhihirisha, kuwa Rais Magufuli alikuwa makini kwenye kuifanya kazi hiyo ya uteuzi.Ona, uteuzi wa Dr Augustino Mahiga kama Waziri wa Mambo ya Nje. Ni kwa kuangalia hali iliyopo kwenye Ukanda wetu na dunia pia.

Kuna changamoto nyingi, ikiwamo ya Ugaidi. Kuna migogoro mingi yenye kuhitaji upatinishi. Tanzania, huko nyuma imekuwa na jukumu la' Kaka Mkubwa' anayefuatwa na mataifa mengine kuombwa ushauri au kuingia kwenye upatanishi kwa migogoro yao. Mtu wa aina ya Augustino Mahiga ni chaguo sahihi la kufanywa Waziri wa Mambo ya Nje mwenye jukumu pia la kuitangaza nchi kimataifa na kuitetea inapobidi.

Uwezo na sifa hizo anazo Augustino Mahiga.Na Baraza la Mawaziri kimsingi ni Baraza la Washauri pia kwa Rais. Ni muhimu kwa aliye madarakani kuwateua wale ambao anaamini pia watakuwa wa msaada mkubwa katika kumshauri. Na Waziri wa Serikali ni waziri wa Nchi nzima. Kumekuwa na dhana ya Waziri kutarajiwa kufanya upendeleo kwa alikotoka. Hayo ni mapungufu.

Pamoja na kuwa ni Baraza dogo la Wizara 18 na mawaziri 34, lakini, tumeliona Baraza lililo na mchanganyiko wenye siha na linaweza kuwa kama shamba lenye matunda ya aina mbali mbali. Ndio, ni Baraza lenye mawaziri wenye uzoefu mbali mbali na wa vizazi tofauti. Ni mawaziri wanaoweza kujifunza mengi kutoka miongoni mwao. Kujifunza yale yanayoweza kuwasaidia kwenye kazi zao.

Maana, katika mseto huo murua wa Baraza, tunaliona, kuwa ni Baraza lenye, hadi sasa, wanawake saba. Ni Baraza lenye vijana wa kizazi Cha Azimio la Arusha, miongoni mwao ni mawaziri wa aina ya Simbachawene na Hussein Mwinyi. Na kuna mawaziri waliozaliwa baada ya Azimio la Arusha, ni mawaziri wa aina ya Angela Kairuki na January Makamba.

Na kuna mawaziri pia waliozaliwa kabla ya Uhuru, ni mawaziri wa aina ya Charles Mwijage na Harrison Mwakyembe.Watanzania wanaelewa, kuwa Rais wao Magufuli hakuwa na sababu wala hakupaswa, katika Baraza hilo dogo na la muhimu kwa taifa, kuwateua mawaziri kwa vigezo vya kanda wanazotoka, dini zao, makabila yao au rangi zao.

Hilo limemsaidia Rais John Magufuli kutoka na Baraza Dogo la kihistoria kwa kwa na hata Waziri mlemavu wa ngozi.
Kilichotegemewa na ndicho kilichotokea, ni Rais Magufuli kuwateua mawaziri wake kwa kuangalia mahitaji ya Watanzania, kisha , kuwatafuta wenye sifa na uwezo wa kutekeleza yale ambayo Watanzania wanayataka kwa maendeleo yao. Na katika hilo la mwisho, Watanzania hawatazami dini, kabila au rangi ya mtu, bali ni Utanzania wa mtu huyo kwa maana ya uzalendo na utendaji wake wa kazi.Maggid,
 
Kumbe Hii Ndio Tafsiri Ya Baraza Dogo La Mawaziri!!.
 
Hivi baraza dogo la mawaziri 19 wala si 18 ukijumlisha na manaibu wao watafika zaidi ya watu 30,baraza lenye watu 30 ni baraza dogo ??? Ebu tafakarini hili.
 
ilitakiwa wawe mawaziri wanne tu...Balaza la watu 34 bado kubwa sana.
 
Baada ya mda mrefu na umakini Rais amemteua Mwakyembe?

Baraza dogo lakini walemavu wana wizara yao na wazee na watoto wizara yao?
 
Hivi baraza dogo la mawaziri 19 wala si 18 ukijumlisha na manaibu wao watafika zaidi ya watu 30,baraza lenye watu 30 ni baraza dogo ??? Ebu tafakarini hili.

Tafsiri hiyo inapatikana Tanzania tu
 
Tafsiri hiyo inapatikana Tanzania tu

Kwa akili za watanzania wakiambiwa ni dogo watalilinganisha na lile la Mr. Fast jet ila tukirudi kwny uhalisia tulitakiwa tuwe na waziri tu ambaye ni mtendaji pia ama tubaki na katibu mkuu pekee ambaye atakuwa pia na political responsibility ikibidi ila kuwa na waziri,naibu waziri,katibu mkuu na naibu katibu mkuu wizara moja ni utaahira mtupu.
 
Back
Top Bottom