Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Mabingwa wa kutukana matusi mitandaoni, vijana wa Chama cha mapinduzi CCM, mngeanza kujitukana wenyewe leo basi, kabla hamjaanza kumshangilia Rais Magufuli kwa kumuondoa kazi aliyekuwa waziri wa nishati na madini Pro. Muhongo (Mb).
Wapinzani tulipoisukuma serikali wakati wa sakata la Escrow, kwamba imuwajibishe Pro. Muhongo, mlikaza mishipa ya shingo kumtetea na kumsifu kwamba ni Jembe, mzalendo msomi na mchapa kazi. Leo mmekuwa kama Bendera fuata upepo.
Uundaji wa kamati za ...kuchunguza wizi kuhusu madini tumelisema sana, lakini CCM imekuwa na kiburi kuliko hata ibilisi. Hotuba mbalimbali zilizowasilishwa na wasemaji wa kambi ya upinzani bungeni zimekuwa zikikataliwa kwa kisingizio kwamba zina uchochezi, uchochezi kwasababu tu zimeandika ukweli wa wizi katika sekta ya madini, lakini watanzania walikuwa wanaona. Leo tunashuhudia yale yale yaliyopiganiwa na wapinzani miaka mingi, tunampongeza na kumtukuza mtu mmoja kama kwamba mambo haya ni mapya.
Laiti kama ushauri wetu ungelikuwa unasikilizwa na kufanyiwa kazi, nchi hii ingefika mbali sana, lakini tumefika hapa kwasababu ya kiburi cha serikali ya CCM, na ushabiki wa wabunge wa chama hicho na wanachama wake wanaodumisha fikra za Mwenyekiti wao.
Watanzania lazima wafahamu kwamba, serikali inaweza kuyakusanya madini, kama ilivyofanya kwenye makusanyo ya mapato, ikajilimbikizia yenyewe, na wananchi wasinufaike hata kidogo, na umasikini ukaendelea kushamiri.
Nawakumbusha tena tafsiri sahihi ya UZALENDO, kwamba ni; Kuilinda nchi yetu Tanzania dhidi ya serikali hii ya CCM.