Wazo jema sana.
Kuna utafiti wa namna ya kutengeneza chakula cha samaki kwa kutumia mti wa muhogo na majani yake na jinsi ya kuumiksi na mlonge alifanya Dr. Nazael Madalla, nana ulikuwa utafiti makini sana.
Lakini kama unavyosema, umeishia kwenye makabati hakuna cha maana ulichokifanya kwa wakulima, japo taabu ya protini kwa ajili ya vyakula vya samaki iko pale pale.
Cha ajabu pamoja na kwamba mihogo inapatikana bong hapa hapa, na milonge longe iko hapa hapa, ilibidi utafiti ukafanyikie Ulaya.
Tanzania bado tuna safari ndefu sana, ila ipo siku tutafika.