Heri ya siku ya kuzaliwa CCM .
Leo chama cha mapinduzi kimetimiza miaka 41 tangu kuasisiwa kwake. Ni umri mkubwa ambao vijana wengi tunaoishi sasa tulizaliwa tukakikuta chama hiki.
Moja ya nguvu kubwa ya chama hiki ni muundo wake unaotambaa kila mahali katika nchi hii na kwenda mpaka ngazi ya chini kabisa ukilinganisha na vyama vingine vya siasa hapa Tanzania.
Lakini pili utaratibu /utamaduni wake wa kubadili Uongozi mara kwa mara kukidhi mahitaji ya Nyakati, umeendelea kukipa uhai na taswira mpya inayowavutia wengi.
Wakati kikiadhimisha umri huo wa miaka 41 ni vyema kujitafakari namna chama kinavyowaandaa makada wake kutoa uongozi mzuri kwa taifa na chama.
Kuna tofauti kubwa kati ya mtu aliyeandaliwa kuwa kiongozi na mtu ambaye imetokea tuu amekuwa kiongozi.
Utaratibu wa kuwapa mafunzo ndani na nje ya nchi ,kuwapa nafasi ndani na nje ya serikali na kuwatizama kwa muda mrefu wanachama watakaotoa uongozi mzuri kwa Taifa na chama bado ni mwafaka katika kuandaa viongozi.
Tuendelee kujenga mifumo mizuri ya kubaini na kuwaendeleza wanachama wenye uwezo na vipaji vya uongozi.
Tuendelee pia kufanya maamuzi ndani ya vikao yanayotokana na mijadala inayotoa fursa kwa kila mtu kuwa huru na kueleza maoni na mtazamo wake kabla ya kufikia uamuzi .Hoja yenye nguvu ndiyo inayoshinda bila kujalisha ameitoa nani.
Isitokee mtu au kikundi fulani cha watu wakajifanya chama ni mali yao, wakitakacho wao ndo hicho hicho, kuwa na maoni tofauti nao ni usaliti na ukosefu wa uzalendo .Hapo chama kitaharibikiwa .
Happy Birthday ccm .
Japhari Mtoro .
Mwanachama wa CCM toka Singida .
5/02/2018 .
0714195367 .