Tafakari yangu juu ya viongozi wetu

Tafakari yangu juu ya viongozi wetu

Molaro

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2013
Posts
818
Reaction score
577
Napata shida sana kuamini elimu za viongozi wetu katika srikali hii ya awamu ya nne imejaa viongozi wenye kiwango kikubwa cha elimu hasa shahada ya uzamivu au maarufu kama PhD.

Kubwa linalonishangaza ni maamuzi yanayochukuliwa na wasomi wanaotegemewa na nchi. Napata shaka na elimu yao hasa pale ninapokumbuka kwamba wengine ni madokta na maprofessa lakini wenye kuchukua maamuzi mabovu ambayo naweza kuyafananisha na maamuzi ya mtoto wa darasa la nne.

Kwanza nianze na sekta ya elimu ambayo kwa sasa iko taabani hasa kwa ngazi ya shule ya msingi na sekondari. Mtakumbuka kuwa wizara ya elimu ilikuwa ikiongozwa na Prof.Jumanne Maghembe ambaye atakumbukwa vyema kwa kufuta kufeli kwa mitihani ya kitaifa ya darasa la nne na kidato cha pili mwaka 2008. Athari za kufuta mitihani hiyo ilikuja kuonekana vyema kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka jana 2012 ambako aslimia 60 ya watahiniwa waliangukia pua. Sina hakika kwamba wale wanaofeli kwa daraja sifuri huwa wanakwenda wapi hasa ukizingatia kuwa serikali huwa inawasahau na bahati mbaya wazazi pia huwatelekeza na kushindwa kuwapa njia mbadala ya elimu.

Ni dhahiri kuwa hili ni kundi kubwa linaloathirika na mfumo wa elimu wa nchi hii unaoandaa wafanyakkazi badala ya waajiri. Haya ndio matunda ya kufuta eleimu ya kujitegemea iliyoasisiwa na mwalimu J.K.Nyerere. Maamuzi mengine mabovu ya majuzi ya kuandaa madaraja mapya yanayoonekana kuwa ni ya chini zaidi ya yote duniani kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi. Maamuzi haya yananipa shaka kwamba wanaoyatoa maamzi haya kama wanashirikisha akili zao na kiwango chao cha elimu au la!!Wizara ya elimu inaongozwa na PhD holders ambao wanatoa maamuzi yanayokinzana. Napata wakati mgumu kutabiri maisha ya kizazi hiki kinachopokea elimu isiyokidhi mahitaji hasa ukizingatia kuwa wanaotoa maamuzi haya walisomeshwa enzi za Mwl Nyerere. Nadhani wanafanya haya kwa sababu watoto wao wanasoma nje ya nchi.

Wizara ya nishati na madini nayo inakuruika katika maamuzi yake na kutoa kejeli kwa wazawa wachache wanaoonesha nia ya kuwekeza katika uchimbaji wa gesi asilia. Sijui anataka rasilimali za nchi hii ziwanufaishe raia wa nchi gani kama siyo watanzania?Shahada alizopata hazimfanyi afikirie kidogo kuhusu Taifa lake?Eti Watanzania wana hela za kuwekeza kwenye juisi tu….kweli!!!!???Hawa ndio wasomi wetu.

Wizara ya Kilimo nayo yanipa shida sababu inakimbilia kuanzisha miradi mipya huku ikiacha ya zamani ambayo nayo kwa kiasi kikubwa ilitumia fedha za wavuja jasho wa nchi hii. Kinachonishangaza ni kila siku kuja na kauli mbiu mpya eti mara MAPINDUZI YA KIJANI,ooohh KILIMO KWANZA na sasa ni MATOKEO MAKUBWA SASA(BIG RESULTS NOW).Nchi ya kauli mbiu iliyokosa watendaji wenye dira.

Viongozi wengi wa nchi hii hawajielewi,napata shida na jinsi walivyopata viwango vya elimu walivyo navyo.Ni nani tutamlaumu kwa kuandaa taifa tegemezi tena lililokata tamaa ya maisha?Je tutawezaje kushindana katika soko la ajira la kimataifa ikiwa hatuna chochote ambacho tunaweza kukifanya vema?Elimu yetu majanga matupu,utalii,ardhi imebinafsishwa,mashirika ya umma yameuzwa,mizigo ya kodi inabebeshwa maskini ambao wengi wao hawaijui kesho yao huku matajiri wakizidi kuneemeka. Haya maamuzi yote yanafaywa na wanasiasa wasomi wa nch hii,wakivurunda hawataki kuwajibika. Wanashindwa kudhibiti uuzaji wa mihadarati kwa vijana ambao ndio nguvukazi taifa,Je wanatuandalia taifa la mateja?

Je ni siasa au ni ulimbukeni tu wa viongozi wetu??Wanatugawa kwa misingi ya dini,makabila na ukanda .Watanzania tuamkeni na tupambane na mifumo mibovu katika nchi hii kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijavyo,Wasomi na wenye maono amkeni na muwafumbue macho watanzania waliovaa miwani ya mbao na pamba maskioni huku wakifurahia usingizi mnono kama wa Pono.

Ni akheri kuongozwa na na mwenye elimu ndogo ambaye ana maamuzi yenye tija kuliko kuongozwa na wasomi ambao wana maamuzi yasiyo na tija kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom