..tafakari ya leo..

SI unit

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
1,953
Reaction score
767
..imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu..
.
.
Ukiwa kama mfanyakazi katika taasisi au shirika flan, unapata majaribu mengi, mfano kufanya jambo lisilo na maslahi kwa shinikizo la miungu watu (mabosi).. Je unachuka hatua gani kusimamia haki?
.
.
Baba familia unaisujudu nyumba ndogo yako na kusahau familia yako kwa "ulaghai" wa hicho kimada chako.. Eti anakupa raha kedekede, lol.. Unakumbuka kiapo cha ndoa yako?
.
.
Patamu ni pale unapoenda kwa waganga eti kuweka mambo sawa.. Itakuaje pale unatoka kwa mganga hata nyumbani hufiki, una R.I.P ukiwa njiani, hayo mambo yako yamekuwa sawa?
.
.
..usimjaribu Bwana Mungu wako, mwabudu yeye peke yake..
.
.
........
Jumapili njema!
 
Vipi wale wanaoenda kwa waganga kutafuta utajiri; shetani angewaonesha milki yote ya duniani na kuwapa iwapo tu watamsujudia.
Wangapi wanaua albino kwa ajili ya .000000000001% ya milki ya dunia?
Wangapi wanajiunga na freemason kwa ajili ya chembe ndogo ya milki ya dunia?
Wangapi wanasababisha wagonjwa wanakufa hosptl kwa ajili ya kujinufaisha juu ya kamchanga kamoja ka milki ya dunia?
Wangapi, wangapi, wangapi?
Na kama boss wao shetani, wanasahau muumba wa mbingu na nchi ni Yesu Kristu ambaye shetani anamjaribu kisa, ana njaa baada ya kufunga siku 40. Na pia hao wafuasi wa shetani au hawajui au wanasahau kuwa wafuasi wa Kristu walifanywa kuwa warithi na wana halali wa Mungu; hivyo milki ya dunia ni yao.
 
.

Asante kwa tafakari nzuri mkuu
 
Ila mauaji ya Kasisi yameniumiza sana leo! Tuwaombee mahalifa wa mitume walioko Zanzibar kwa kweli.
.
Huu ni mpango mkakati wa shetani kupitia hao wafuasi wake wanaovaa vibaraghashia.
:
Ila imeandikwa, ...na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, na wala milango ya kuzimu haitalishinda...
:
Amin nakwambia mwisho wao upo karibu!
 
ila mauaji ya kasisi yameniumiza sana leo! Tuwaombee mahalifa wa mitume walioko zanzibar kwa kweli.
siyo wewe tu, yamegusa hisia za wakristo wote na kusababisha huzuni na hasira, pamoja na hofu... Maombi tu hayatoshi hatuna budi kujibu mashambulizi kwa style nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…