Tafakari ya leo, (be authentic)


Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Messages
1,211
Likes
434
Points
180
Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2012
1,211 434 180
Asubuhi njema wanamafanikio,
Tumeianza siku hii nyingine nzuri kwetu, siku mpya ambapo tumepata nafasi ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tunachofanya ili tuweze kupata katokeo bora.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu uhalisia,
Tunapokuwa tunakitaka kitu kwa hamu na shauku kubwa, tupo tayari kufanya chochote ili tupate kile tunachotaka.
Tupo tayari kuigiza na kudanganya ili tu tupate kile tunachotaka.
Unamwambia mteja vitu ambavyo unajua haviwezekani ili tu akubali kununua au kulipia huduma fulani.
Kwenye usaili wa kazi unasema vitu ambavyo unajua kabisa huwezi kufanya lakini unawadanganya ili wakupe kazi.
Kwenye mahusiano unadanganya ili ukubaliwe na wengine, kama ni uchumba unaweza kuigiza mpaka kubadili dini ili tu upate kile unachotaka.

Ni kweli utapata kile unachotaka kwa njia hii, lakini hakitadumu kwa muda mrefu, watu wataona ukweli halisi na hawatafurahia kuendelea kuwa na wewe.
Kama ni biashara wateja wataona ukweli kwamba ulichoahidi hujatimiza na hivyo watakwenda kwingine.
Kama ni kazi ufanisi wako utaonesha wazi kwamba huwezi kufanya kama ulivyoahidi.
Kama ni mahusiano, ukishapata kile ulichotaka changamoto ndipo zinaanza na watu kushutumiana kwamba wamebadilika..

Dawa ya kuondokana na yote haya ni kuwa halisi, ahidi kile unachoweza kutimiza, fanya kile unachoweza kufanya. Usiahidi hovyo, usidanganye wala usiigize. Ishi kama ulivyo wewe, na utawavutia wale wanaoendana na wewe.
Unapokuwa halisi unawavutia wale ambao wako halisi kuwa na wewe. Unapokuwa feki utawavutia walio feki pia na hamtakwenda kwa muda mrefu.
Kuwa halisi, kuwa wewe, hapo ndipo mafanikio yako yalipo.
Nakutakia siku njema sana,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

#MUHIMU; Karibu tufanye kazi pamoja, bonyeza link hii kupata maelekezo; www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
 
hydroxo

hydroxo

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Messages
1,208
Likes
1,269
Points
280
hydroxo

hydroxo

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2015
1,208 1,269 280
Ujumbe mzuri wenye mazingatio.

Ingawa wanadamu wa sasa,wengi wao hawaaminiki.

Uongo,usengenyaji,utapeli,wizi,kuigiza maisha vimekuwa vitu vinavyosumbua mno.

Na kadri unavyotoa nasaha,kwa mtu ama kundi moja anaibuka ama linaibuka kundi lingine doing the same thing.

It is just you fight with mythical hydra.

Cha muhimu tusichoke kupeana nasaha na kukumbushana kuishi vyema tena kwa uhalisia.
 
Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Messages
1,211
Likes
434
Points
180
Makirita Amani

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2012
1,211 434 180
Ujumbe mzuri wenye mazingatio.

Ingawa wanadamu wa sasa,wengi wao hawaaminiki.

Uongo,usengenyaji,utapeli,wizi,kuigiza maisha vimekuwa vitu vinavyosumbua mno.

Na kadri unavyotoa nasaha,kwa mtu ama kundi moja anaibuka ama linaibuka kundi lingine doing the same thing.

It is just you fight with mythical hydra.

Cha muhimu tusichoke kupeana nasaha na kukumbushana kuishi vyema tena kwa uhalisia.
Hakika.
 
baracuda

baracuda

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Messages
767
Likes
435
Points
80
baracuda

baracuda

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2014
767 435 80
Ujumbe murua sana..ubarikiwe.
 

Forum statistics

Threads 1,238,798
Members 476,185
Posts 29,330,975