Tafakari Fupi Kuhusu Mke

Jeho

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
5,068
Reaction score
5,559
Kuna mjadala miongoni mwa watu mitaani kuhusu mke, utasikia mke ni nani yako? Na majibu wengine husema ni rafiki, wengine husema ni ndugu. Wakati mwingine mke amechukuliwa kama asiye thamani maana wanadai wakati wowote unaweza ukaachana naye kwa hiyo si vizuri akajua mambo yako yote. Huo ni mtazamo kulingana na Dunia, lakini kulingana na Muumbaji wetu, mke anatajwa kama ifuatavyo.

Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana angawa yeye ni mwenzako na mke wa agano lako(Malaki 2:14).

Penye rangi nyekundu panabainisha wazi kuwa, mke ni mwenzako, na sababu iko wazi kabisa kuwa mke ni matokeo ya ubavu uliotolewa kwa mme, na hivyo kama ni ubavu ni sawa na wewe. Hivyo unavyomtendea mambo ya ajabu ni sawa na kwamba unajitendea mwenyewe maana huo ndio ubavu wako, labda kama ni ubavu wa mwingine. Na kwa wale wanaodiriki kuucha ubavu na kuuacha ukitangatanga pengine, Mungu anaonya hivi

Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli….
(Malaki 2:15,16).

Na hata zama za Yesu Kristo alikumbusha hilo pale alipoulizwa swali kuhusu kumuacha mke kwa kumpa talaka, na alijibu hivi

Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi
(Mathayo 19:8).

Nilikuwa nakumbusha tu, maana kizazi hiki cha nyoka hakioni ajabu kutenda mambo kinyume na ilivyokusudiwa tokea awali.
 
Ni kweli kabisa mke na mume ni mwili mmoja,kwanini umtendee mabaya mume au mke wako wakati ni sehemu ya mwili wako? Yaan nikitafakari hili hata kama mume wangu kaniudh vipi namsamehe nikichukulia tu ni kama mguu wangu umejikwaa nikaanguka je niuchukie mguu wangu?
 

Una akili sana!!!
 
Nampenda sana mke wangu, na nikosoma maneno kama haya nampenda zaidi, naamini Mungu anafurahi nikimpenda mke wangu. Naamini nitafika mbinguni kwa kuipenda familia yangu. Raha tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…