Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora kamanda wa polisi mkoani humo,Kamishina Msaidizi Mwandamizi Willbroad Mtafungwa amesema kuwa, baada ya kufanyika msako huo na upelelezi dhidi yao waganga hao wengine wamebainika kupiga ramri chonganishi na wengine kufanya shughuli hizo bila kibali.
Aidha katika hatua nyingine Kamanda wa polisi amesema kuwa,kumezuka vikundi vya vijana waarifu ambao wamekuwa wakiwapora wananchi mali zao huku wakiwajeruhi kwa vitu vyenye ncha kali wanaojiita changia dogo,ambapo wamekamatwa viijana wapatao 17,watafikishwa mahakamani kutokana na kukiri makosa yao.
Chanzo: ITV