GE2025 Tabora: Sita mbaroni kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,160
Reaction score
11,228

Vyombo vya usalama mkoani Tabora vimewakamata watu sita kwa tuhuma za kutoa rushwa ya fedha kwa baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wajumbe wa uchaguzi wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuelekea uchaguzi wa wagombea wa madiwani na wabunge ndani ya chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 3, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane katika Wilaya ya Nzega, ambapo watuhumiwa walinaswa wakigawa fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 16 ndani ya gari.

Watuhumiwa waliokamatwa wamemtaja mmoja wa wagombea wa ubunge katika jimbo la Nzega kama mhusika mkuu wa kutoa fedha hizo, ambaye kwa sasa ametoweka huku akiendelea kusakwa.

Ameongeza kuwa zaidi ya watu 40 wengine bado wanasakwa kwa tuhuma hizo huku akitoa wito kwa wagombea wote kujiepusha na vitendo vya rushwa, akisisitiza kuwa vyombo vya dola vimejipanga kushughulikia yeyote atakayekiuka sheria au taratibu za uchaguzi.

Katika Jimbo la Nzega, wagombea sita wa CCM wanachuana kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Chanzo: Jambo Tv
 
Kazi nzuri..nahao zaidi ya 40 wakipatatika mtuletee taarifa..hatuwezi kufumbia macho Rushwa...Na mikoa mingine tunahitaji taarifa za Rushwa na hatua mnazochukua..
 
Ndo maana mnaambiwa wekeni reforms....viongoz wa kwel wapatikanike....kiongoz anatoa Rushwa achaguliwe...unafikir akikamata usukan.ataacha kuiba....ataacha kugawa rasilimal kwa wageni....we need reforms
 
Vyombo vya usalama mkoani Tabora vimewakamata watu sita kwa tuhuma za kutoa rushwa ya fedha kwa baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wajumbe wa uchaguzi wa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuelekea uchaguzi wa wagombea wa madiwani na wabunge ndani ya chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 3, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane katika Wilaya ya Nzega, ambapo watuhumiwa walinaswa wakigawa fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 16 ndani ya gari.

Watuhumiwa waliokamatwa wamemtaja mmoja wa wagombea wa ubunge katika jimbo la Nzega kama mhusika mkuu wa kutoa fedha hizo, ambaye kwa sasa ametoweka huku akiendelea kusakwa.

Ameongeza kuwa zaidi ya watu 40 wengine bado wanasakwa kwa tuhuma hizo huku akitoa wito kwa wagombea wote kujiepusha na vitendo vya rushwa, akisisitiza kuwa vyombo vya dola vimejipanga kushughulikia yeyote atakayekiuka sheria au taratibu za uchaguzi.

Katika Jimbo la Nzega, wagombea sita wa CCM wanachuana kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Chanzo: Jambo Tv
Unafiki tuu rushwa aliyo itoa mwenye kiti hamkuiona
 
Back
Top Bottom