sizonjemadawa
JF-Expert Member
- Feb 11, 2017
- 1,053
- 1,304
Ni kawaida kwa mzazi akiwa na mtoto zaidi ya mmoja, kuwalinganisha hasa tabia zao, tangu pale walipozaliwa., Utakuta huyu alikuwa analia sana , labda huyu alikuwa analala sana huyu ni mpole au huyu ni mtundu n.k
Hata hivyo watoto hao wanapozidi kukuwa tabia na maumbile yao huzidi kutofautiana siku hadi siku. Mara nyingi muonekano wao hutofautiana kiasi kwamba ni vigumu kutambua kuwa ni watoto wa mama na baba mmoja.
Katika miaka mingi watafiti wemegundua kuwa kuna uhusiano mkubwa wa tabia za watoto na mpangilio wa kuzaliwa. Kwa mfano watoto wa kwanza kuzaliwa,mtoto wa pili, na wamwisho.
Mtoto wa kwanza.
Mtoto wa kwanza katika familia mara nyingi anawajibika juu ya wenzake,anakuwa na mpangilio wa mambo yake,huwa anafanikiwa katika mambo yake, na huwa anonyesha mfano mzuri wa kuwa kiongozi mbele ya wadogo zake.
Yeye huwa anakuwa ndiye kinara wa tabia njema au anayefanya vitu ambavyo wazazi huwa wanapenda, na mara nyingi anafanya hivyo kama mfano kwa wadogo zake.kama kuna watoto wadogo hapo nyumbani mtoto wa kwanza anakuwa kama yeye ndio mlezi na wadogo zake wanapenda kujifunza kutoka kwake
Mara nyingi wanakuwa na malengo ya kufanya vizuri shuleni na marazote wanapata mafanikio kwa sababu wanajitahidi sana.Kwa bahati mbaya mara nyingine kwa sababu ya kutaka sana kufanikiwa kunamsababishia msongo wa mawazo ambao si vizuri sana kwa watoto.
Mtoto wa kati
Mtoto wa katikati mara nyingi anachukuliwa kuwa mtoto mgumu sana kumuelewa, Mara nyingi mtoto huyu hapati nafasi ya kupendwa kama alivyokuwa mtoto wa kwanza au wa mwisho, huwa anaona anatengwa na ni vigumu sana kwake kuona ni mwelekeo upi aende.
Na mara nyingi anakuwa na mtazamo tofauti wa nini afanye au nani awe, ili kujitofautisha na mkubwa wake, na mara nyingi huwa ni mtafiti na huwa anapenda kujaribu vitu ambavyo ni vigumu kujua matokeo yake.
Mtoto wa mwisho
Mtoto wa mwisho ni mtoto wa familia, ni mtoto ambaye kila mmoja ndani ya familia anawajibika kumuangalia. Wazazi wanapenda kumpendelea na mara nyingi zile sheria wazazi walizoweka huwa kwa mtoto huyu wa mwisho azizingatiwi tena.