Tabia ya watu wa 'pinga pinga'

Kuna upuuzi umeibuka wa watu kusifia kila kitu hata vile ambavyo havina faida yoyote kwa Taifa.

Huu upuuzi unataka Taifa zima tufanane akili tuwe ni watu wa kusifu tu.

Nasema huu ujinga ukome mara moja.
wanaosifu na wanaopinga kila kitu wote wanaumwa aina moja ya ugonjwa nao unaitwa njaa.

mmoja njaa inakula tumbo vibaya,mwingine imehamia kichwani.
 
Waliosema flyover zisijengwe maana vijijini hakuna maji uliwaelewa?
Lazima mambo yote yaende kwa usawa.
Uko sio kupinga bali kutoa mawazo mbadala kwasababu yote hayo lazima yangekuja kufanyika,sasa inategemea aliyeshika mpini kipaumbele chake ni nini.Anayesifia ndiye mwenye matatizo makubwa zaidi kwasababu anasifia kitu ambacho ni wajibu wa mtu kukifanya.serikali inafanya mambo kwasababu ni wajibu sio hisani.
 
Wanaosifu kila kitu hao ni wasaka vyeo na teuzi na wameshashtukiwa.
Mimi naongelea suala la kupinga kila jambo jema. Kila kitu kinachoanzishwa wanasema hicho hatuwezi

Huwa mnaongea uongo mwingi wa kijinga mpaka inatokea watu wanakosoa na kupinga mengi ya mambo yenu. Kwa mfano sasa inasemekana rais atatoa 600,000b kwenye hospitali ya muhimbili! Isitoshe hao unaosema kila kitu chao kinapingwa, wao huwa wanaunga mkono kila kitu? Hebu tuanzie hapo.

Halafu inaonekana ww ni bendera fuata upepo ndio maana unatumia neno kupinga kila kitu, wakati hakuna anayepinga kila kitu, bali kukosoa aprroach ya mambo mengi.
 
Mkuu Usisahau na "Royal Tour"...waliipinga ila sasa tunaona manufaa yake..watalii wamefurika🐒
Tena ilikuwa inapingwa na lile Genge la Kihutu.

Tunapinga FAKE NEWS kama mlivyotaka kutuaminisha kuhusu ule upumbavu wa lile Gazeti la Scotsland na ile Fotoshop
 
Kiukweli JPM ni habari nyingine, ndio maana sisi wengine tulishauri hata miaka 10 haitoshi!, na tukapendekeza hatuna hata haja ya kufanya uchaguzi wa rais Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
P
Mungu akatengua upumbavu wenu na taaluma za mitihani,huwezi kumpangia Mungu,kila mtu ni sawa chini ya jua,oh sijui bila fulani nchi haiwezi kusonga huo ni upumbavu na msirudiea tena,acheni dhambi,acheni kupora uchaguzi,acheni uchama ninyi,acheni ukabila,acheni ukanda,acheni dharau,MUNGU HADHIHAKIWI.
 
Wanaosifu kila kitu hao ni wasaka vyeo na teuzi na wameshashtukiwa.
Mimi naongelea suala la kupinga kila jambo jema. Kila kitu kinachoanzishwa wanasema hicho hatuwezi

Ninadhani wewe ni mmoja wa wanaoamini kuwa binadamu wote huwaza sawa. Au anayeamini kuna njia moya TU ya kufanya jambo fulani.

Ni kweli nimesikia mambo hayo yakipingwa lakini SIO umuhimu au uwepo wake. Kuoinga kumehusu jambo moja - CHANZO CHA FEDHA!! Wakati tukiambiwa “fedha zetu za ndani” watu wengi waliaminishwa ni makusanyo ya mapato ya ndani. Kumbe walimaanisha mikopo kwa kuwa tutailipa wenyewe basi ni fedha zetu!!

Wengi wa waliopinga walitaka au PPP model au mikopo ya riba nafuu. Tukachukua mikopo ya kibiashara kwa sababu tulikuwa tunaambiwa watoa riba nafuu ni “mabeberu”.

Binadamu wana mawazo tofauti tofauti. Hatuwazi sawa. Hata hao usiotaka wapingwe wanawaza tofauti na wapinzani wao! Haina maana kuwa wako sahihi au sio sahihi. Acha kuwaona wako sahihi ndio utaelewa umuhimu wa kuwa na fikra tofauti!!!
 
Yaani serikali isifiwe kwa kodi za wananchi?

Yaani serikali isifiwe kwa kupeleka maji mahali ambayo ni kodi ya wananchi?

What a shame.
 
Maelezo yako ni ya kiataarabu sana! Nayapenda hata kama ningekuwa sikubaliani nayo. Wengi wetu humu ndani hawajui dunia iliendeleaje tukafika hapa tulipo. Mawazo mapya huboreshwa ikiwa na upande wa pili wa wazo lako la awali utatilia maanani. Vinginevyo dunia hii ingekuwa kama meza badala ya kuwa mduara mpaka kesho.

Sent from my ONEPLUS A5000 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…