Tabia hii haifai.

Kyenju

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2012
Posts
5,143
Reaction score
2,547
Mtu uko kwenye daladala unaandika sms au unachart na mtu, kwenye kiti ulichokaa kuna abiri mwenzako na nyuma ya kiti chako kuna abiria wengine. Wote utaona macho wameyatoa shingo wamezirefusha kila mmoja anataka asome unachokiandika, wanakunyima uhuru wa kuandika unachokiandika, abiria tuache tabia hii.
 
Kweli kabs hii tabia inakera, sasa ukiona hivyo dawa yao ni ndogo sn me huwa nikishaona wananichungulia huwa ninaandika bonge la tus then unajifanya kama unawanyanyulia sm ili wasome vizur unawawekea kwa mda ili wasome vizur, hizi ni tabia za kishenz sna, hawa wanafanana na watu wanaotuchunguliaga madirishan au vyoon

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Wewe ni kiboko yao.
 
Inanikumbusha story moja jamaa alikua anaandika msg kama kawaida pembeni kuna mdada amekaa katoa macho kama kabanwa na mlango akadiriki kumwambia jamaa umekosea..'kaka umekosea sio...' just imagine mpaka mtu anadiriki kusoma msg yako na kujua kama umekosea..unajua kilichofuata?
 
dawa yao unaandika ' nitakujibu baadae kuna w****** wametoa mijicho kusoma msg yangu....uone watakavyozodoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…