Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,423
.........."Wakati wa matayarisho ya Mapinduzi ya 1964 Abeid Karume alikuwa mwenyekiti wa kamati ya watu kumi na nne waliokuwa wakipanga Mapinduzi kwa siri chini ya Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam, Lakini nyuma ya pazia Mwalimu Nyerere naye alikuwa akiratibu mapinduzi ya Zanzibar kupitia kwa John Okello ambayo kimsingi ndio yaliyofanikiwa kutukia yakiratibiwa kwenye mashamba ya mkonge katika kijiji cha Kipumbwi Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.
Akiwa na umri wa miaka 59, Karume alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vilevile kubaki na wadhifa wake wa Rais wa Afro- Shirazi Party, Haya mambo yote yalifanyika mjini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa leo ujulikanao kama uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliungana hapo tarehe 26 Aprili,1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 27Aprili,1964.
Kinadharia sababu za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinaweza kutazamwa katika jicho la udugu tu, lakini hoja hii inaweza kuvunjwa na hoja ya kuwa ikiwa kama ni udugu ni sababu tosha basi Rwanda na Burundi ndizo zingekuwa na hoja hii ya kurejea Tanganyika kwakuwa zilikuwa ni moja ya mikoa ya Tanganyika kabla ya vita vya pili vya dunia zilipochukuliwa na koloni la Ubelgiji. Kuna sababu kuu tatu ambapo zimefanyiwa utafiti na kudhihirika zilifanya kazi mpaka kutimia kwa Muungano huu.
1. Mwalimu Julius Nyerere aliamini na ilikuwa sahihi Zanzibar ni eneo muhimu la kimbinu hasa katika nyakati za ukombozi wa Afrika na mpaka sasa, na njia zaidi za udhibiti wa mamlaka lilikuwa chaguo sahihi kuzidhibiti Zanzibar, Comoro na Ushelisheli ambako hadi sasa ni maeneo muhimu kwa maslahi ya Tanzania na vizazi vijavyo kiasi kwamba mwelekeo wa nchi hizo huamuliwa kutokea Dodoma na Dar es Salaam nchini Tanzania. Hata baada ya safari yake ya kwanza ya Rais Nyerere nchini China kwa Mao, Shirika la Ujasusi la MSS la China lilichagua ardhi ya Zanzibar kuwa kituo chao kikuu cha Ujasusi Afrika.
2. Abeid Amani Karume kwakuwa Madaraka aliyapata toka mikononi mwa Julius Nyerere pale uwanja wa ndege Ukonga jijini Dar es Salaam, salama yake dhidi ya mabwana wa mapinduzi hasa wale wafuasi wa John Gideon Okello ambao wengi walikuwa wanamtii, ilikuwa ni kujiunga na Tanganyika ili kulindwa na Julius Nyerere. Muungano kwake ilikuwa hoja Muhimu.
3. Ethan Sanders kutoka Bridgewater State University katika utafiti wake aliouita Conceiving the Tanganyika-Zanzibar Union in the Midst of the Cold War: Internal and International Factors analitaja shirika la ujasusi la CIA la Marekani kwamba liliratibu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Marekani ilikuwa kwenye vita baridi na Ujamaa toka Muungano wa Kisoviet, katika vita ya kuuzima ujamaa usiingie Kenya na Uganda kisha ukasambaa Afrika, njia ya dharula ilikuwa ni muungano huo, hivyo wakainjinia Muungano, Katika ripoti hiyo anawanukuu Prof Haruob Othuman na Prof Issa Shivji ambao wanarejea nyuma kidogo kwenye mapinduzi na kuonyesha mashirika ya Italia-SISMI, Uingereza-M16 na Marekani-CIA yalifahamu mapinduzi hayo. Hivyo misukumo yote hii ilizaa Muungano.
Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulikuwa nguzo muhimu kwa Karume kujijenga mamlakani. Ili kusafisha njia na kuondoa uchafu aliyouona unamghasi, aliona ni vyema awasambaratishe kwa kuwatafutia nafasi za uongozi Tanzania Bara ambako wasingeweza kufurukuta. Waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Abdulrahman Babu (Umma Party) na Uwaziri wa Mipango na Uchumi kwenye Serikali ya Muungano, Kassim Hanga (ASP) akateuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri, na Mambo ya Muungano na Salim Ahmed Salim (Umma Party) aliteuliwa kuwa Balozi nchini Misri.
Wengine ni Othman Sharrif (ASP) aliyeteuliwa Balozi nchini Marekani, lakini Karume akampinga Mwl. Nyerere akidai hastahili, uteuzi ukafutwa. Badala yake akateuliwa kuwa Afisa Mifugo katika moja ya mikoa ya Kusini Tanzania, Mbeya au Mtwara, na Kanali Ali Mahfoudh (Umma Party) akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Operesheni/Mazoezi katika Jeshi la Wananchi (JWT).........."
Kitabu: Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi
Sura ya 1.
Ukurasa 126.